Social Icons

Pages

Friday, 25 July 2014

LA LIGA: RATIBA MSIMU MPYA YATOKA, SUAREZ KUMALIZIA KIFUNGO ‘EL CLASICO’!



RFEF, Shirikisho la Soka Spain, Leo limetangaza Ratiba ya La Liga kwa Msimu mpya wa 2014/15 na Vigogo, Real Madrid watakuwa Wenyeji wa Barcelona hapo Oktoba 26 kwenye Mechi ambayo huenda ikawa ya kwanza kwa Luis Suarez kwa Timu yake Barca baada ya kumaliza Kifungo chake cha Miezi Minne.
SUAREZ-IN-BARCALigi hiyo itaanza Wikiendi ya Agosti 23 na Mabingwa Watetezi, Atletico Madrid, wataanza na Rayo Vallecano.
Real Madrid na Barcelona zote zitaanzia Nyumbani kwa Real kucheza na Cordoba na Barca kuivaa Elche.
Kwenye Ratiba ya ufunguzi, Sevilla watakuwa Nyumbani kucheza na Valencia ikiwa ni kama Marudiano ya Fainali ya EUROPA LIGI ya Msimu uliopita.
Pia Wikiendi hiyo itakuwepo Dabi ya Jiji la Vila-real kati ya Levante na Villareal wakati Malaga wataanza na Athletic Bilbao ndani ya La Rosaleda.
Mechi ya Marudiano ya El Clasico itakuwa huko Camp Nou wakati Barcelona watakapoikaribisha Real hapo Machi 22, 2015.
LA LIGA
Mechi za Ufunguzi Msimu mpya 2014/15
Wikiendi Agosti 23-24
Sevilla-Valencia
Barcelona-Elche
Rayo Vallecano-Atlético de Madrid
Eibar-Real Sociedad
Real Madrid-Córdoba
Celta-Getafe
Levante-Villarreal
Málaga-Athletic Club
Almería-Espanyol
Granada-Deportivo

FRANK LAMPARD AJIUNGA NEW YORK CITY!



FRANK_LAMPARDKiungo wa zamani wa Chelsea Frank Lampard amejiunga na Klabu itakayocheza Major League Soccer, MLS, huko Marekani New York City FC kwa Mkataba wa Miaka Miwili.
Lampard, mwenye Miaka 36, alimaliza Mkataba wake na Chelsea mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya kuwa Klabuni hapo kwa Miaka 13.
Lampard alihamia Chelsea kutoka West Ham Juni 2001 kwa Uhamisho wa Pauni Milioni 11 na kuweka Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Chelsea kwa kufunga Mabao 211 katika Mechi 649.
New York City FC, ikiwa inamilikiwa na Manchester City, ni Klabu mpya iliyoanzishwa hivi karibuni na itashiriki MLS Mwakani na hivi sasa ndio imeanza kusajili Wachezaji na tayari imeshamnasa Straika wa zamani wa Spain David Villa kutoka Klabu ya Spain Atletico Madrid.
Lakini Villa, mwenye Miaka 32, atacheza kwa Mkopo huko Australia kwenye Klabu ya Ligi A Melbourne City kuanzia Oktoba hadi Desemba na inaaminika Lampard huenda akafuata njia hiyo hiyo.

LAMPARD-Mataji:
-LIGI KUU ENGLAND: 2004-05, 2005-06, 2009-10
-FA Cup: 2006-07, 2008-09, 2009-10, 2011-12
-Ligi Cup: 2004-05, 2006-07
-UEFA Championz Ligi: 2011-12
-Europa Ligi: 2012-13

Hivi sasa Ligi ya MLS inajijenga kwa kuchukua Mastaa mbalimbali kwenye Klabu zao mbalimbali.
Baadhi ya Mastaa hao ni Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Thiery Henry, anaechezea New York Red Bulls, Jermain Defoe, aliekuwa Tottenham, na sasa yuko Toronto FC, Tim Cahill kutoka Everton yuko New York Red Bulls, Obafemi Martins, aliekuwa Newcastle, yupo Seattle Sounders pamoja na Clint Dempsey wakati Robbie Keane, aliewahi kuzichezea Liverpool na Tottenham, yupo LA Galaxy.
Vile vile Staa wa Brazil, Kaka, anatarajiwa kujiunga na Orlando City Mwakani.

VAN GAAL AKIRI UHABA WA MASENTAHAFU



Louis van Gaal amekiri kuwa Kikosi chake kina uhaba wa Wachezaji kwenye Difensi baada ya kulazimika kumtumia Kiungo Darren Fletcher kama Sentahafu kwenye Mechi waliyoichapa LA Galaxy Bao 7-0.
LVG-ROONEY-MAZOEZINI-USAMeneja huyo mpya wa Manchester United katika Mechi yake ya kwanza kabisa alitumia Mfumo wa 3-5-2 na kuanza na Mabeki Watatu ambao ni Jonny Evans, Chris Smalling na Phil Jones.
Baada ya Mapumziko, Chipukizi Tyler Blackett na Michael Keane waliungana na Nahodha Darren Fletcher kwenye Difensi na kumudu kutofungwa hata Bao kwenye Mechi hiyo iliyochezwa huko Rose Bowl, Pasadena.
Kufuatia kung’atuka kwa Nemanja Vidic, alieenda Inter Milan, na Rio Ferdinand, aliekwenda QPR, Masentahafu wamekuwa adimu.
Akiongea na MUTV, Kituo cha TV cha Man United, Van Gaal alikiri: “Sina Mabeki wa ziada. Hivyo ikabidi nimweke Mchezaji [Fletcher] ambae ameifanya kazi lakini hafai nafasi hiyo.”
Hata hivyo, Van Gaal ameridhika na jinsi Wachezaji wake wanavyokubali mafunzo yake na amesema Chipukizi Reece James, aliefunga Bao 2, anapaswa kufurahia mafanikio hayo katika Mechi yake ya kwanza.
Van Gaal ameeleza: “Nilikuwa na Siku 3 tu na Kundi hili. Mazoezi ya kwanza hayakuwa mazuri lakini ya pili yalikuwa afadhali sana. Hivyo wanaendelea vizuri na nasikia fahari kuwa na Vijana hawa.”
Aliongeza: "Ukisikiliza vizuri, utacheza vizuri na Reece James ni Kijana mdogo mwenye kipaji kikubwa. Natumai anaweza kucheza hivi katika Gemu nyingi kama hivi!"

NI MPYA HII, CITY YASAINI MCHEZAJI KWA VIDEO!



MABINGWA wa England Manchester City wamedaiwa kutoa Mkanda wa Video ukionyesha Beki wa FC Porto Eliaquim Mangala akisaini kujiunga na Klabu hiyo.
Eliaquim-MangalaMangala, Beki wa France mwenye Miaka 23, amekuwa akihusishwa na City kwa muda mrefu katika kipindi hiki cha Uhamisho na aliwahi kuonekana Jijini Manchester lakini hakuna tamko rasmi ambalo limetolewa hadi sasa.
Hata hivyo, Mkanda wa Video kwenye Tovuti ya Man City ulimuonyesha Mchezaji huyo akitua Jijini Manchester na Ndege maalum na kupokewa rasmi na kisha kupimwa afya yake.
Lakini Man City imekanusha Video hiyo na kudai Tovuti yao iliingiliwa na ‘Wavamizi’ na kuweka taarifa ambazo si za kwao.
Mangala alikuwemo kwenye Kikosi cha France huko Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia lakini hakucheza hata Mechi moja.
Man City
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
13 Julai Dundee 2-0 Man City
18 Julai
Heart of Midlothian 1-2 Man City (Sinclair, Kolarov)
23 Julai
Sporting Kansas 1 Man City 4, Kansas, USA
Guinness International Champions Cup
27 Julai
AC Milan v Man City, Heinz Field, USA
30 Julai
Liverpool v Man City, New York, USA
2 Agosti
Olympiacos v Man City, Bank Stadium, USA
Ngao ya Jamii

10 Agosti Man City v Arsenal, 17.00, Wembley Stadium fulu viwanja blogspot.com

Wednesday, 23 July 2014

LVG KUANZA NA LA GALAXY, BECKHAM AITEMBELEA MAN UNITED!



WAKATI himaya mpya ya Meneja mpya Louis van Gaal inaanza Asubuhi ya Jumatano huko LVG-NAMBA1Pasadena Rose Bowl kwa Washabiki 70,000 kufurika kuiona Manchester United ikicheza na Los Angeles Galaxy, Mchezaji wa zamani wa Timu hizo mbili David Beckham alitembelea Hoteli ya Beverly Hills kuwasabahi Marafiki zake wa Man United.
Beckham, Lejendari wa Man United, yuko huko Los Angeles kwa matembezi na alifika Hotelini na kuongea na Wachezaji wa Man United na Mameneja wao, Louis van Gaal na Ryan Giggs, ambae waliwahi kucheza pamoja huko Man United tangu wakiwa wadogo.
Ingawa Mechi hii ni ya Kirafiki, ila mwishoni Mshindi hutunzwa Chevrolet Cup, Mashabiki wa Man United wanaifuatilia kwa hamu kuona Van Gaal anaanza vipi wadhifa wake.
Wiki nzima kwenye Mazoezi Man United wamekuwa wakitumia Mfumo wa 4-3-3 na huenda wakautumia kwenye Mechi na LA Galaxy.
LVG-GIGGS-BECKHAM
Vile vile, Wadau watakuwa na udadisi mkubwa nani atateuliwa kuwa Nahodha wa Mechi hiyo huku Kura kubwa ikienda kwa Wayne Rooney.
Lakini pia mvuto ni kuwaona Wachezaji wapya, Ander Herrera na Luke Shaw, wakivaa Jezi ya Man United kwa mara ya kwanza.
Mmoja wa Wachezaji wa LA Galaxy ambae Man United watamjua vizuri ni Mchezaji wa zamani wa Tottenham na Liverpool ambae sasa ni Nahodha wa Republic of Ireland, Robbie Keane.
Baada ya Mechi hii, Man United watasafiri kwenda Miji ya Denver, Washington na Detroit kucheza na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid kwenye Mashindano ya International Champions Cup

STAA WA BARCA ATUA STOKE, CAULKER AMFATA RIO QPR, ULLOA YU LEICESTER



PATA MPYA ZA UHAMISHO LIGI KUU ENGLAND:
STAA WA BARCA ATUA STOKE
Bojan-KrkicBojan Krkic, ambae ni mzao wa La Masia na ambae kuna wakati alifananishwa na Lionel Messi huko Barcelona, amesaini kuichezea Stoke City kwa Dau la Pauni Milioni 3 kwa Mkataba wa Miaka Minne.
Krkic atajiunga na Kikosi cha Mark Hughes Usiku huu tayari kwa Ziara yao ya Germany kwa Mazoezi na Mechi za Kirafiki.
Krkic, Miaka 23, alipimwa afya na kukubaliana kujiunga na Stoke Wiki mbili zilizopita lakini Klabu yake Barcelona ilisita kukamilisha Uhamisho wake.
Kijana huyo alikuzwa kutoka Chuo cha Vijana maarufu cha Barcelona, La Masia, ambacho ndicho kilichowakomaza kina Messi, Andrés Iniesta na Xavi, na akaweza kuichezea Timu ya Kwanza ya Barca akiwa na Miaka 17 tu hapo Septemba 2007.
Baadae akapelekwa kucheza kwa Mkopo huko Italy kwa Klabu za AS Roma na AC Milan na kisha kuichezea pia Ajax ya Holland.
Kuhusu kumnasa Staa huyo, Mark Hughes, ambae mwenyewe aliwahi kuichezea Barcelona, amesema: "Mtu yeyote anaejua Soka la Ulaya lazima atamjua huyu kama Mchezaji na kuichagua Stoke hii inafurahisha sana na kuifanya Klabu ikubalike!"
STEVEN CAULKER AJIUNGA QPR TOKA CARDIFF
QPR imemsaini Beki wa Cardiff City Steven Caulker kwa Dau ambalo halikutajwa.
Caulker, Miaka 22, alijiunga na Cardiff, ambayo sasa imeporomoka Daraja toka Ligi Kuu England Mwaka Jana, mwanzoni mwa Msimu wa 2013/14 akitokea Tottenham.
Huko QPR ataungana na Beki mkongwe Rio Ferdinand ambae amesainiwa Juzi tu kama Mchezaji Huru baada ya kuondoka Manchester United.
Caulker alicheza huko Tottenham chini ya Meneja Harry Redknapp ambae sasa ni Meneja wa QPR.
Akizungumzia uamuzi wake kujiunga na QPR, Caulker alieleza: “Harry ndio sababu kubwa na Rio pia ni kivutio. Ilikuwa muhimu kwangu kurudi kucheza Ligi Kuu England!”
Msimu uliopita Caulker aliichezea Cardiff  Mechi zake zote 38 za Ligi na kufunga Bao 5 lakini Timu hiyo ikashushwa Daraja na kutupwa Championship baada kumaliza Mkiani.
Caulker ameichezea England mara moja, Novemba 2012, na kufunga Bao moja wakati England ilipochapwa 4-2 na Sweden katika Mechi ya Kirafiki.
LEONARDO ULLOA AJIUNGA LEICESTER CITY KWA £8M ABAYO NI REKODI!
Leicester City wamemsaini Straika wa Brighton Leonardo Ulloa kwa Dau la Pauni Milioni 8 ambayo ni Rekodi kwa Klabu hiyo kumnunua Mchezaji kwa Bei ghali.
Dau kubwa walilowahi kulipa Leicester ni Pauni Milioni 5.5 walipomnunua Ade Akinbiyi Julai 2000.
Ulloa, mwenye Miaka 27, ni Raia wa Argentina ambae aliifungia Brighton Bao 16 Msimu uliopita.
Brighton wamesema ilibidi wakubali kumuuza kwa Dau ambalo ni Rekodi pia kwao kwa mauzo kwa vile Mchezaji huyo alikazania kucheza Ligi Kuu England.
Ulloa alijiunga na Brighton kutoka Klabu ya Spain Almeria Januari 2013 kwa Dau la Pauni Milioni 2.
Leicester City wamepanda Ligi Kuu England Msimu huu mpya baada kutwaa Ubingwa wa Daraja la Championship

VPL: USAJILI WAONGEZWA WIKI 2, KWISHA AGOSTI 17!



TAIFA STARS KUPIGA KAMBI MBEYA
UWANJA_WA_TAIFA_DARKikosi cha Taifa Stars kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Mbeya ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji.
Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini Julai 31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto.
…MECHI YAINGIZA SHILINGI MILIONI 158
Mechi ya michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh. 158,350,000 kutokana na washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama za mchezo sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 74,432,095.
Tunawashukuru washabiki wote waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
MUDA WA USAJILI WAONGEZWA KWA WIKI MBILI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili kwa wiki mbili ili kuzipa klabu nafasi ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa. Hivyo hatua ya kwanza ya usajili inakamilika Agosti 17 mwaka huu badala ya Agosti 3 ya awali.
Kutokana na marekebisho hayo, kipindi cha uhamisho kinakamilika Agosti 17 mwaka huu wakati pingamizi itakuwa kati ya Agosti 19 hadi 26 mwaka huu.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itathibitisha usajili kati ya Septemba 1 na 2 mwaka huu.
Uhamisho wa kimataifa, usajili wa wachezaji huru, na utatuzi wa dosari za usajili unatakiwa uwe umekamilika kufikia Septemba 7 mwaka huu. Uthibitisho wa hatua ya mwisho ya usajili utafanywa Septemba 15 mwaka huu.
Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015 itaanza Septemba 20 mwaka huu, na ratiba itatolewa mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo.

PATRICK VIEIRA AVUNJA MECHI YA MAN CITY U-21 HUKO CROATIA SABABU YA UBAGUZI!



MABINGWA wa England Manchester City wamevunja Mechi yao ya Vijana wa chini ya Miaka 21, U-21, dhidi ya HNK Rijeka huko Novigrad, Croatia hapo Jana kwa madai ya kukashifiwa Kibaguzi kwa mmoja wa Wachezaji wao.
SEKO-FOFANAWakati Mechi ikivunjika, City walikuwa mbele kwa Bao 1-0 na walitoka nje mara tu baada ya Kiungo wao, Seko Fofana, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada kumtandika Teke mpinzani lakini inaaminika hiyo ni sababu ya kukashifiwa.
VIEIRA
Lakini kila upande umetoa taarifa tofauti kwa Man City kudai kuwa katika Kipindi cha Kwanza Uongozi wao ulilazimika kuitoa nje Timu yao kufuatia kukashifiwa Kibaguzi kwa Mchezaji wao anaeaminika kuwa ni Seko Fofana, Raia wa France.
Timu ya HNK Rijeka imedai kuwa Kocha wa Man City, Patrick Vieira, aliingia Uwanjani na kuongea na Refa na, kwa mshangao wa wengi, kuamua kuitoa nje Timu yake bila wao kujua ni kwa sababu gani.
Fofana, ambae huchezea France U-19, alijiunga na City Januari 2013 akitokea Klabu ya Ligue 1 huko France, FC Lorient.
Januari 2013, AC Milan walivunja Mechi yao ya Kirafiki dhidi ya Timu ya Daraja la chini huko Italy, Pro Patria, baada ya Mashabiki kumpigia kelele za Kibaguzi Mchezaji wao Kevin-Prince Boateng ambae aliukamata Mpira na kuubutua kwa Mashabiki hao na kisha kuongoza Timu yake kutoka nje na Mechi kuvunjika.

Tuesday, 22 July 2014

Timu za jeshi zapaswa wekewa mikakati ili kuleta ushindani”- Juma Nkamia

“Timu za jeshi zapaswa wekewa mikakati ili kuleta ushindani”- Juma NkamiaTimu za Jeshi ambazo zilishiriki ligi kuu msimu uliopita ni JKT Ruvu,Ruvu Shooting,Mgambo JKT,Rhino Rangars na JKT Oljoro kati ya hizo mbili za Oljro na Rhino zimeshuka daraja
NAIBU waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Tanzania Juma Nkamia amelishauri Shirikisho la soka nchini TFF,kuishauri bodi ya Michezo ya Jeshi la kujenga Taifa JKT,kuwa na timu chache kwenye ligi kuu ambazo zitamudu ushindani.
Nkamia alisema Jeshi hilo limekuwa na timu zisizopungua tano kwenye ligi kuu ya Tanzania bara inayoshirikisha timu 14 lakini ni timu mbili peke zinazo mudu ushindani kwenye ligi hiyo zilizobaki zimekuwa kama wasindikizaji jambo ambalo ameliita ni sawa na ubadhilifu wafedha.
“Itapendeza kuona kama TFF,itaketi na wenzetu wa Jeshi la JKT,na kuweka mikakati ya kuwa na angalau timu mbili kwenye ligi kuu ambazo zitaandaliwa vizuri na kutoa ushindani wa kweli kwenye ligi tofauti na hivi sasa ambapo jeshi hilo lina timu tano ni zote hazina mwenendo mzuri kwenye ligi.
Timu za Jeshi ambazo zilishiriki ligi kuu msimu uliopita ni JKT Ruvu,Ruvu Shooting,Mgambo JKT,Rhino Rangars na JKT Oljoro kati ya hizo mbili za Oljro na Rhino zimeshuka daraja huku Mgambo ya Kabuku Tanga ikiponea chupuchupu kushuka daraja.

Stars bado ina nafasi ya kufuzu”- Mart Nooij

“Stars bado ina nafasi ya kufuzu”- Mart NooijKatika mchezo wa marudiano Stars italazimika kushinda idadi kubwa ya mabao zaidi ili kusonga mbele hatua ya makundi.
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Satrs’Mart Nooij,amesema kikosi chake bado kina nafasi ya kucheza hatua ya makundi katika kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika licha ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Msumbiji jana.
Nooij ameiambia Goal kwamba matokeo hayo siyo mazuri kwa Stars lakini atahakikisha anazitumia vizuri dakika 90 za Maputo kwa ajili ya kikosi chake kucheza hatua ya Makundi.
“Nikweli sare ya 2-2 nyumbani siyo matokeo mazuri kwetu lakini hatutalala tuta tutahakikisha tunakwenda kupambana Maputo na kupata ushindi kama tulivyo fanya Harare kwenye mechi yetu na Zimbabwe.
Katika mchezo wa marudiano Stars italazimika kushinda idadi kubwa ya mabao zaidi ili kusonga mbele hatua ya makundi.

YANGA YAMPA MKATABA JAJA

Jaja alizaliwa Septemba 21 mwaka 1985 huko Brazili na kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa mfungaji bora katika timu aliyokuwa akiichezea ya Itabaina FC iliyopo Kitongoji cha Sergipe.
Yametimia klabu ya soka ya Yanga imempa mkataba wa miaka miwili mshambuliaji raia wa Brazili Geilson Santana Santos ‘Jaja’ huku Mganda Hamis Kiiza ‘Diego’akitarajiwa kutupiwa virago ili klabu hiyo ibakiwe na nyota watano wakigeni kama Sheria za TFF,zinavyoagiza.
Jaja aliyekuja Tanzania wiki iliyopita kwa ajili ya majaribio anakuwa mchezajI wa pili kutoka Brazili kusaini Yanga baada ya Andrey Coutinho, kusaini mkataba wa muda kama huo wiki tatu zilizopita.
Katibu Mkuu wa Yanga Beno Njovu aliiambia fulu viwanja Jaja amekuwa na juhudi kubwa kwenye mazoezi ya timu hiyo kiasi cha kumvutia kocha Maximo na kuamua kumpa mkataba huo wa miaka miwili japo hakusema dau ambalo wamemchulia.
“Nikweli Jaja tumempa mkataba wa miaka miwili baada ya kumaliza mazoezi ya asubuhi baada ya kocha Maximo kuridhishwa na kiwango chake,”alisema Njovu.
Jaja alizaliwa Septemba 21 mwaka 1985 huko Brazili na kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa mfungaji bora katika timu aliyokuwa akiichezea ya Itabaina FC iliyopo Kitongoji cha Sergipe nchini Brazili.

UEFA CHAMPIONZ LIGI: LEO MARUDIANO RAUNDI YA PILI



Mechi za Marudiano za Raundi ya Pili ya Mtoano za UEFA CHAMPIONZ LIGI zitachezwa Leo hii Jumanne na Kesho Jumatano.
UCL-2014-15-LOGOWashindi wa Raundi hii tayari wanajua nani Wapinzani wao wa Raundi ya Tatu ya Mtoano baada ya UEFA kufanya Droo yake Ijumaa iliyopita.
Washindi wa Raundi ya Tatu ya Mtoano watasonga Raundi ya Mwisho ya Mtoano ambayo ndio hatua ya mwisho kabla Mechi za Makundi kuanza.
Raundi ya Tatu ya Mtoano imepangwa kwenye Makundi mawili, yale ya Njia ya Mabingwa na jingine Njia ya Ligi, ambapo wale Washindi 10 wa Njia ya Mabingwa watapambanishwa wenyewe kwa wenyewe kwenye Raundi ya Mwisho ya Mtoano wakati wale Washindi Watano wa Njia ya Ligi watapangwa na Timu 5 zinazoanzia Raundi hiyo ambazo ni Arsenal FC, FC Porto, Bayer 04 Leverkusen, SSC Napoli and Athletic Club.
Washindi 10 wa Raundi ya Mwisho ya Mtoano watajumuika na Klabu 22 zilizoingizwa moja kwa moja, wakiwemo Mabingwa Real Madrid, kwenye Droo ya kupanga Makundi 8 ya Timu 4 kila moja.
UEFA CHAMIPONZ LIGI
Raundi ya Pili ya Mtoano
RATIBA
**Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Jumanne Julai 22
1830 Sutjeska Niksic V Sheriff Tiraspol (0-2)
1900 F91 Dudelange V Ludogorets Razgrad (0-4)
1900 Levadia V Sparta Prague (0-7)
1930 FK Qarabag V Valletta FC (1-0)
2030 Maccabi Tel Aviv V FC Santa Coloma (1-0)
2045 The New Saints V Slovan Bratislava (0-1)
2100 HB Tórshavn V Partizan Belgrade (0-3)
2100 Skënderbeu Korcë V BATE Borisov
2115 Zalgiris V Dinamo Zagreb (0-2)
2130 Debrecen V Cliftonville
2145 Celtic V KR Reykjavík (1-0)
Celtic Vs KR Reykjavík
Jumatano Julai 23
1800 Aktobe V Dinamo Tbilisi (1-0)
1900 HJK Helsinki V Rabotnicki (0-0)
1900 Ventspils V Malmö FF (0-0)
2030 Steaua Bucharest V Strømsgodset (1-0)
2100 NK Maribor V Zrinjski Mostar (0-0)
2145 St Patrick's Athletic V Legia Warsaw (1-1)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Tatu ya Mtoano
(Mechi kuchezwa 29/30 Julai na Marudiano ni 5/6 Agosti)
Njia ya Mabingwa

Valletta FC (MLT)/Qarabağ FK (AZE) v FC Salzburg (AUT)
Cliftonville FC (NIR)/Debreceni VSC (HUN) v FC BATE Borisov (BLR)/KS Skënderbeu (ALB)
ŠK Slovan Bratislava (SVK)/The New Saints FC (WAL) v FC Sheriff (MDA)/FK Sutjeska (MNE)
Aalborg BK (DEN) v GNK Dinamo Zagreb (CRO)/VMFD Žalgiris (LTU)
Legia Warszawa (POL)/Saint Patrick's Athletic (IRL) v KR Reykjavík (ISL)/Celtic FC (SCO)
FC Dinamo Tbilisi (GEO)/FK Aktobe (KAZ) v Strømsgodset IF (NOR)/FC Steaua Bucureşti (ROU)
HŠK Zrinjski (BIH)/NK Maribor (SVN) v FC Santa Coloma (AND)/ Maccabi Tel-Aviv FC (ISR)
FK Rabotnicki (MKD)/HJK Helsinki (FIN) v APOEL FC (CYP)
AC Sparta Praha (CZE)/FC Levadia Tallinn (EST) v Malmö FF (SWE)/FK Ventspils (LVA)
PFC Ludogorets Razgrad (BUL)/F91 Dudelange (LUX) v FK Partizan (SRB)/HB Tórshavn (FRO)

Njia ya Ligi
AEL Limassol FC (CYP) v FC Zenit (RUS)
FC Dnipro Dnipropetrovsk (UKR) v FC København (DEN)
Feyenoord (NED) v Beşiktaş JK (TUR)
Grasshopper Club (SUI) v LOSC Lille (FRA)
R. Standard de Liège (BEL) v Panathinaikos FC (GRE)

**TIMU 13 ZITAKAZOINGIA MOJA KWA MOJA RAUNDI YA TATU YA MTOANO:
-APOEL
-Red Bul Salzburg
-Aab
-Zenit Saint Petersburg
-Lille
-Copenhagen
-Standard Liège
-Beşiktaş
-Dnipro Dnipropetrovsk
-Panathinaikos
-Feyenoord
-Grasshoppers
-AEL Limassol

MATS HUMMELS AKARIBIA KUTUA MANCHESTER UNITED!



UPO uwezekano mkubwa kwa Sentahafu wa Germany na Klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels kujiunga na Manchester United kabla Wikiendi hii kufika.
MATS-HUMMELSHivi sasa Klabu hizo mbili zipo kwenye mazungumzo mazito lakini habari zilizovuja zimedai makubaliano yatafikiwa hivi karibuni.
Hummels, mwenye Miaka 25, aling’ara huko Brazil wakati Germany ilipotwaa Kombe la Dunia kwa kuichapa Argentina Bao 1-0 kwenye Fainali iliyochezwa Julai 13 huko Maracana, Rio de Janeiro.
Ikiwa Uhamisho huu utakamilika, Hummels atakuwa Mchezaji wa 3 kununuliwa na Meneja mpya Louis van Gaal, baada ya Ander Herrera na Luke Shaw, lakini umuhimu wake ni mkubwa sana kwani Man United imeshapoteza Mabeki wazoefu watatu walioondoka, ambao ni Nemanja Vidic, Rio Ferdinand na Patrice Evra, na kuja kwake kutaimarisha safu ya ulinzi.
Pia, kuja kwa Mjerumani huyo kutawapa moyo sana Mashabiki wa Man United baada ya Jana Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Klabu hiyo, Ed Woodward, kusema wategemee Wachezaji wapya katika Wiki chache zijazo.
Woodward alitamka: “Hamna kiwango cha Bajeti kilichowekwa. Kifedha tuna nguvu sana, zipo Fedha za Uhamisho. Louis ndie Bosi na anatathmini nini kinaendelea lakini tumekuwa na mazungumzo na walengwa na kazi inaendelea nyuma ya pazia. Tunasonga mbele kwa baadhi ya walengwa hao…hivyo kaeni chonjo hapa!”
Aliongeza: “Louis anapata muda zaidi wa kufanya tathmini yake na ikibidi tutabadilisha maamuzi na kufanya mengine. Tunataka kuchukua hatua thabiti ili kutwaa Ubingwa!

ROONEY: ‘TUNATAKA TUMVUTIE MENEJA MPYA



WAYNE ROONEY ana nia kubwa ya kuonyesha uwezo wake kwa Meneja mpya wa Manchester United, Louis van Gaal, wakati wakiwa huko Marekani kwenye Ziara yao.
Van Gaal, ambae alitambulishwa rasmi kama Meneja mpya Alhamisi iliyopita, alisema hivi sasa kazi yake kubwa ni kutathmini Kikosi kilichopo na kuamua nani abaki na wapya gani waletwe.
LVG-ROONEY-MAZOEZINI-USAIngawa Rooney hategemewi kuwa mmoja wa wale waliopo kwenye mashaka hayo, Fowadi huyo ameapa kujituma zaidi ili kumwonyesha uwezo wake Van Gaal.
Rooney amesema: “Lazima tuonyeshe uwezo wetu kila Siku kwenye Mazoezi kama Wachezaji na Timu. Kila mmoja anataka amvutie Meneja mpya na hilo ndio lengo letu!”
Lakini pia Rooney amevutiwa mno na Van Gaal na ameeleza: “Ilikuwa vyema tulipokutana na Meneja mpya na Wasaidizi wake. Vipindi vya kwanza vya Mazoezi vilikuwa safi na kila mmoja anangojea kwa hamu kucheza Mechi! Tunae Meneja mpya mwenye mtazamo tofauti na lazima tufanye Mazoezi vizuri na kusikiliza nini anataka sisi tufanye na kulifanya hilo uwanjani na kumwonyesha uwezo wetu.”
Man United watacheza na Los Angeles Galaxy Jumatano kugombea Chevrolet Cup huko Los Angeles na kisha kusafiri kwenda Miji ya Denver, Washington na Detroit kucheza na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid kwenye Mashindano ya International Champions Cup.
Ingawa Mechi za Ziara kabla Msimu mpya kuanza huchukuliwa kirahisi kama vile sehemu ya Mazoezi, Rooney anaamini Wiki mbili zijazo ni muhimu kwa Msimu wao mpya na amesema: “Kila Mchezaji atakueleza kitu muhimu katika Msimu ni kupata matayarisho mazuri kabla Msimu mpya kuanza.”
International Champions Cup
MAKUNDI
KUNDI A:
-Manchester United
-AS Roma
-Real Madrid
-Inter Milan
KUNDI B
-AC Milan
-Olympiacos
-Manchester City
-Liverpool
RATIBA
**Saa zikitajwa ni za Bongo
Ijumaa Julai 25
03:00 Olympiacos CFP v AC Milan
Jumamosi Julai 26
23:10 Manchester United v AS Roma
Jumapili Julai 27
1:00   Real Madrid CF v Inter Milan
23:00 AC Milan v Manchester City
Jumatatu Julai 28
02:00 Liverpool - England v Olympiacos CFP
Jumatano Julai 30
02:00 Manchester United v Inter Milan
05:15 Real Madrid CF v AS Roma
Alhamisi  Julai 31
02:00 Manchester City v Liverpool
Jumamosi Agosti 2
20:00 Inter Milan v AS Roma
22:00 Olympiacos CFP v Manchester City
23:06 Manchester United v Real Madrid CF
Jumapili Agosti 3
01:30 Liverpool v AC Milan
FAINALI
Jumatatu Agosti 4
Mshindi Kundi A v Mshindi Kundi B..........fulu viwanja blogspot.com

WACHEZAJI 6 WA SHAKHTAR DONETSK WAGOMA KURUDI ‘VITANI’ UKRAINE!



COSTA-TEIXEIRAWACHEZAJI 6 wa Shakhtar Donetsk wamekataa kurudi Mji wa Donetsk huko Ukraine kutokana na Vita ya wenyewe kwa wenyewe Nchini humo.
Mji wa Donetsk uko kwenye eneo linalomilikiwa na Waasi wanaoungwa mkono na Urusi huku Jeshi la Ukraine likipigana kutaka kulikomboa.
Klabu ya Shakhtar Donetsk ilikuwa huko France Wikiendi iliyopita kucheza Mechi ya Kirafiki na Lyon lakini Wachezaji Alex Teixeira, Fred, Dentinho, Douglas Costa, Facundo Ferreyra na Ismaily waligoma kurudi Ukraine.
Rais wa Klabu hiyo ambae pia ndie Mmiliki wake, Rinat Akhmetov, amewaonya Wachezaji hao kwamba wataadhibiwa vikali.
Amesema: “Wachezaji wana Mikataba ambayo inabidi waiheshimu. Kama hawarudi wao ndio watakuwa wa kwanza kuumia.”
Nae Meneja wa Shakhtar anaetoka Romania, Mircea Lucescu, amemlaumu Wakala wa baadhi ya Wachezaji hao, Kia Joorabchian, kwa kuwashawishi kugoma kurudi Ukraine.
Meneja huyo amedai Wakala huyo anataka kutumia machafuko ya Ukraine anufaike kwa kuwafanya Wachezaji hao kuwa huru wakati wana Mikataba.
Watano kati ya Wachezaji 6 waliogoma kurudi ni kutoka Brazil na Ferreyra ni Mtu wa Argentina.
Hivi sasa Shakhtar hawaruhusiwi kuutumia Uwanja wao wa Nyumbani, Donbass Arena uliopo Mjini Donetsk, kutokana na Vita hiyo lakini, huku Msimu mpya ukitakiwa kuanza Wikiendi hii, Shirikisho la Soka la Ukraine halijaamua Klabi hiyo itacheza wapi Mechi zake za Nyumbani.fulu viwanja blog spot.com

REAL YAENDA USA NA KIKOSI DHAIFU


fulu viwanja blogspot.com


LEO hii Real Madrid wameruka kwenda Marekani kushiriki International Champions Cup wakiwa na Kikosi dhaifu ambacho kina Wachezaji 9 toka Timu yao B, Castilla.
REAL_MADRID_PLAYERSMbali ya kuwakosa Álvaro Morata na Casemiro ambao Juzi tu wamehama, Real haina hata Mchezaji wao mmoja aliecheza Kombe la Dunia huko Brazil.
Wachezaji wa kwanza wa Real waliokuwa Brazil ambao watajumuika Kikosini Jumatano huko Los Angeles ni Wachezaji wa Spain, Xabi Alonso, Iker Casillas na Sergio Ramos, pamoja na Luka Modric wa Croatia.
Kisha, Siku mbili baadae, watafuatia Wachezaji wa Portugal, Fábio Coentrão, Cristiano Ronaldo na Pepe, lakini Ronaldo atakuwa kwenye Mazoezi maalum binafsi akiendelea kupona Goti lake.
Kundi jingine la Wachezaji wa Kombe la Dunia wa Real ni lile la Wachezaji wao kutoka France, Raphaël Varane na Karim Benzema, na hawa wamepangiwa kurudi Likizo Agosti 1.
Wachezaji waliosalia ni wale Timu zao zilikutana kwenye Fainali ya Kombe la Dunia huko Brazil, Angel Di Maria aliekuwa na Argentina na Toni Kroos na Sami Khedira waliokuwa na Germany, na hawa watajiunga na Real hapo Agosti 5 toka kwenye Likizo zao.
International Champions Cup
MAKUNDI
KUNDI A:
-Manchester United
-AS Roma
-Real Madrid
-Inter Milan
KUNDI B
-AC Milan
-Olympiacos
-Manchester City
-Liverpool
RATIBA
**Saa zikitajwa ni za Bongo
Ijumaa Julai 25
03:00 Olympiacos CFP v AC Milan
Jumamosi Julai 26
23:10 Manchester United v AS Roma
Jumapili Julai 27
1:00   Real Madrid CF v Inter Milan
23:00 AC Milan v Manchester City
Jumatatu Julai 28
02:00 Liverpool - England v Olympiacos CFP
Jumatano Julai 30
02:00 Manchester United v Inter Milan
05:15 Real Madrid CF v AS Roma
Alhamisi  Julai 31
02:00 Manchester City v Liverpool
Jumamosi Agosti 2
20:00 Inter Milan v AS Roma
22:00 Olympiacos CFP v Manchester City
23:06 Manchester United v Real Madrid CF
Jumapili Agosti 3
01:30 Liverpool v AC Milan
FAINALI
Jumatatu Agosti 4
Mshindi Kundi A v Mshindi Kundi B

KITABU CHA SIR ALEX TOLEO JIPYA OKTOBA KUMGUSA MOYES!



KLABU ya Manchester United imetoboa kuwa Sir Alex Ferguson atatoa Toleo jipya la Kitabu cha Maisha yake Mwezi Oktoba Mwaka huu.
ALEX_FERGUSON-MY_AUTOBIOGRAPHYKitabu hicho, 'My Autobiography', kilichapishwa kwa mara ya kwanza Oktoba 2013 na kuvunja Rekodi zote kwa kuwa Kitabu cha kwanza, ambacho si cha Hadithi, kuuza Nakala nyingi na haraka mno katika Historia ya uchapishaji Vitabu.
Sir Alex Ferguson alistaafu kuwa Meneja wa Manchester United Mwezi Mei Mwaka Jana baada ya kuendesha himaya yake kwa mafanikio makubwa kwa Miaka 26.
Toleo hili jipya litaongeza habari za maisha ya Sir Alex tangu astaafu pamoja na mawazo yake kuhusu Manchester United alivyoiona baada ya kustaafu na hasa himaya fupi ya Miezi 10 ya Meneja aliemrithi yeye, David Moyes, ambayo iliivuruga Man United na kuipotezea Ubingwa na pia kuifanya ishindwe kucheza Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 1996 baada ya kumaliza Nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu England.
Pia Toleo hilo jipya litagusia mafundisho yake huko Chuo Kikuu cha Harvard Marekani, Usiku wa Tuzo za Oscar na Tripu yake ya Boti kuzunguka Hebrides, Magharibi ya Pwani ya Scotland.
Hadi sasa hamna fununu yeyote nini kitaandikwa kwenye Toleo hilo jipya, hasa kuhusu kushindwa kwa David Moyes, ambae yeye mwenyewe Sir Alex ndie aliempendekeza.

Hivi sasa Man United ipo chini ya Meneja mpya Louis van Gaal ambae ametoboa yeye na Sir Alex ni Marafiki na wakati wowote ule watakutana kupata Kahawa au Mvinyo pamoja.
Hata hivyo, haijajulikana kama pia Van Gaal nae atatajwa kwenye Toleo hili jipya la Kitabu cha Sir Alex Ferguson, 'My Autobiography
 
FULU VIWANJA