WAKATI Real Madrid wakivuliwa
ubingwa wa kombe la Mfalme jana usiku kufuatia kutoka sare ya 2-2,
mahasimu wao wa jadi FC Barcelona wameishushia Elche CF mvua ya mabao
4-0
Kinyume na matarajio ya wengi,
kocha wa Barca, Luis Enrique alibadili kikosi chake akiwaacha nje Luis
Suarez, Neymar na mfalme wa Camp Nou, Lionel Messi.
Safari hii hakuna aliyelalamika kwani vijana walipiga kandanda la hatari katika mechi hiyo ya robo fainali.

Kwa matokeo hayo Elche wametupwa nje ya michuano kwa wastani wa mabao 9-0 kwani mechi ya kwanza walichapwa 5-0.
