
Baada ya Mapumziko, Chipukizi Tyler Blackett na Michael Keane waliungana na Nahodha Darren Fletcher kwenye Difensi na kumudu kutofungwa hata Bao kwenye Mechi hiyo iliyochezwa huko Rose Bowl, Pasadena.
Kufuatia kung’atuka kwa Nemanja Vidic, alieenda Inter Milan, na Rio Ferdinand, aliekwenda QPR, Masentahafu wamekuwa adimu.
Akiongea na MUTV, Kituo cha TV cha Man United, Van Gaal alikiri: “Sina Mabeki wa ziada. Hivyo ikabidi nimweke Mchezaji [Fletcher] ambae ameifanya kazi lakini hafai nafasi hiyo.”
Hata hivyo, Van Gaal ameridhika na jinsi Wachezaji wake wanavyokubali mafunzo yake na amesema Chipukizi Reece James, aliefunga Bao 2, anapaswa kufurahia mafanikio hayo katika Mechi yake ya kwanza.
Van Gaal ameeleza: “Nilikuwa na Siku 3 tu na Kundi hili. Mazoezi ya kwanza hayakuwa mazuri lakini ya pili yalikuwa afadhali sana. Hivyo wanaendelea vizuri na nasikia fahari kuwa na Vijana hawa.”
Aliongeza: "Ukisikiliza vizuri, utacheza vizuri na Reece James ni Kijana mdogo mwenye kipaji kikubwa. Natumai anaweza kucheza hivi katika Gemu nyingi kama hivi!"