Social Icons

Pages

Tuesday, 22 July 2014

ROONEY: ‘TUNATAKA TUMVUTIE MENEJA MPYA



WAYNE ROONEY ana nia kubwa ya kuonyesha uwezo wake kwa Meneja mpya wa Manchester United, Louis van Gaal, wakati wakiwa huko Marekani kwenye Ziara yao.
Van Gaal, ambae alitambulishwa rasmi kama Meneja mpya Alhamisi iliyopita, alisema hivi sasa kazi yake kubwa ni kutathmini Kikosi kilichopo na kuamua nani abaki na wapya gani waletwe.
LVG-ROONEY-MAZOEZINI-USAIngawa Rooney hategemewi kuwa mmoja wa wale waliopo kwenye mashaka hayo, Fowadi huyo ameapa kujituma zaidi ili kumwonyesha uwezo wake Van Gaal.
Rooney amesema: “Lazima tuonyeshe uwezo wetu kila Siku kwenye Mazoezi kama Wachezaji na Timu. Kila mmoja anataka amvutie Meneja mpya na hilo ndio lengo letu!”
Lakini pia Rooney amevutiwa mno na Van Gaal na ameeleza: “Ilikuwa vyema tulipokutana na Meneja mpya na Wasaidizi wake. Vipindi vya kwanza vya Mazoezi vilikuwa safi na kila mmoja anangojea kwa hamu kucheza Mechi! Tunae Meneja mpya mwenye mtazamo tofauti na lazima tufanye Mazoezi vizuri na kusikiliza nini anataka sisi tufanye na kulifanya hilo uwanjani na kumwonyesha uwezo wetu.”
Man United watacheza na Los Angeles Galaxy Jumatano kugombea Chevrolet Cup huko Los Angeles na kisha kusafiri kwenda Miji ya Denver, Washington na Detroit kucheza na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid kwenye Mashindano ya International Champions Cup.
Ingawa Mechi za Ziara kabla Msimu mpya kuanza huchukuliwa kirahisi kama vile sehemu ya Mazoezi, Rooney anaamini Wiki mbili zijazo ni muhimu kwa Msimu wao mpya na amesema: “Kila Mchezaji atakueleza kitu muhimu katika Msimu ni kupata matayarisho mazuri kabla Msimu mpya kuanza.”
International Champions Cup
MAKUNDI
KUNDI A:
-Manchester United
-AS Roma
-Real Madrid
-Inter Milan
KUNDI B
-AC Milan
-Olympiacos
-Manchester City
-Liverpool
RATIBA
**Saa zikitajwa ni za Bongo
Ijumaa Julai 25
03:00 Olympiacos CFP v AC Milan
Jumamosi Julai 26
23:10 Manchester United v AS Roma
Jumapili Julai 27
1:00   Real Madrid CF v Inter Milan
23:00 AC Milan v Manchester City
Jumatatu Julai 28
02:00 Liverpool - England v Olympiacos CFP
Jumatano Julai 30
02:00 Manchester United v Inter Milan
05:15 Real Madrid CF v AS Roma
Alhamisi  Julai 31
02:00 Manchester City v Liverpool
Jumamosi Agosti 2
20:00 Inter Milan v AS Roma
22:00 Olympiacos CFP v Manchester City
23:06 Manchester United v Real Madrid CF
Jumapili Agosti 3
01:30 Liverpool v AC Milan
FAINALI
Jumatatu Agosti 4
Mshindi Kundi A v Mshindi Kundi B..........fulu viwanja blogspot.com
 
FULU VIWANJA