STAA WA BARCA ATUA STOKE

Krkic atajiunga na Kikosi cha Mark Hughes Usiku huu tayari kwa Ziara yao ya Germany kwa Mazoezi na Mechi za Kirafiki.
Krkic, Miaka 23, alipimwa afya na kukubaliana kujiunga na Stoke Wiki mbili zilizopita lakini Klabu yake Barcelona ilisita kukamilisha Uhamisho wake.
Kijana huyo alikuzwa kutoka Chuo cha Vijana maarufu cha Barcelona, La Masia, ambacho ndicho kilichowakomaza kina Messi, Andrés Iniesta na Xavi, na akaweza kuichezea Timu ya Kwanza ya Barca akiwa na Miaka 17 tu hapo Septemba 2007.
Baadae akapelekwa kucheza kwa Mkopo huko Italy kwa Klabu za AS Roma na AC Milan na kisha kuichezea pia Ajax ya Holland.
Kuhusu kumnasa Staa huyo, Mark Hughes, ambae mwenyewe aliwahi kuichezea Barcelona, amesema: "Mtu yeyote anaejua Soka la Ulaya lazima atamjua huyu kama Mchezaji na kuichagua Stoke hii inafurahisha sana na kuifanya Klabu ikubalike!"
STEVEN CAULKER AJIUNGA QPR TOKA CARDIFF
QPR imemsaini Beki wa Cardiff City Steven Caulker kwa Dau ambalo halikutajwa.
Caulker, Miaka 22, alijiunga na Cardiff, ambayo sasa imeporomoka Daraja toka Ligi Kuu England Mwaka Jana, mwanzoni mwa Msimu wa 2013/14 akitokea Tottenham.
Huko QPR ataungana na Beki mkongwe Rio Ferdinand ambae amesainiwa Juzi tu kama Mchezaji Huru baada ya kuondoka Manchester United.
Caulker alicheza huko Tottenham chini ya Meneja Harry Redknapp ambae sasa ni Meneja wa QPR.
Akizungumzia uamuzi wake kujiunga na QPR, Caulker alieleza: “Harry ndio sababu kubwa na Rio pia ni kivutio. Ilikuwa muhimu kwangu kurudi kucheza Ligi Kuu England!”
Msimu uliopita Caulker aliichezea Cardiff Mechi zake zote 38 za Ligi na kufunga Bao 5 lakini Timu hiyo ikashushwa Daraja na kutupwa Championship baada kumaliza Mkiani.
Caulker ameichezea England mara moja, Novemba 2012, na kufunga Bao moja wakati England ilipochapwa 4-2 na Sweden katika Mechi ya Kirafiki.
LEONARDO ULLOA AJIUNGA LEICESTER CITY KWA £8M ABAYO NI REKODI!
Leicester City wamemsaini Straika wa Brighton Leonardo Ulloa kwa Dau la Pauni Milioni 8 ambayo ni Rekodi kwa Klabu hiyo kumnunua Mchezaji kwa Bei ghali.
Dau kubwa walilowahi kulipa Leicester ni Pauni Milioni 5.5 walipomnunua Ade Akinbiyi Julai 2000.
Ulloa, mwenye Miaka 27, ni Raia wa Argentina ambae aliifungia Brighton Bao 16 Msimu uliopita.
Brighton wamesema ilibidi wakubali kumuuza kwa Dau ambalo ni Rekodi pia kwao kwa mauzo kwa vile Mchezaji huyo alikazania kucheza Ligi Kuu England.
Ulloa alijiunga na Brighton kutoka Klabu ya Spain Almeria Januari 2013 kwa Dau la Pauni Milioni 2.
Leicester City wamepanda Ligi Kuu England Msimu huu mpya baada kutwaa Ubingwa wa Daraja la Championship