
Beckham, Lejendari wa Man United, yuko huko Los Angeles kwa matembezi na alifika Hotelini na kuongea na Wachezaji wa Man United na Mameneja wao, Louis van Gaal na Ryan Giggs, ambae waliwahi kucheza pamoja huko Man United tangu wakiwa wadogo.
Ingawa Mechi hii ni ya Kirafiki, ila mwishoni Mshindi hutunzwa Chevrolet Cup, Mashabiki wa Man United wanaifuatilia kwa hamu kuona Van Gaal anaanza vipi wadhifa wake.
Wiki nzima kwenye Mazoezi Man United wamekuwa wakitumia Mfumo wa 4-3-3 na huenda wakautumia kwenye Mechi na LA Galaxy.

Vile vile, Wadau watakuwa na udadisi mkubwa nani atateuliwa kuwa Nahodha wa Mechi hiyo huku Kura kubwa ikienda kwa Wayne Rooney.
Lakini pia mvuto ni kuwaona Wachezaji wapya, Ander Herrera na Luke Shaw, wakivaa Jezi ya Man United kwa mara ya kwanza.
Mmoja wa Wachezaji wa LA Galaxy ambae Man United watamjua vizuri ni Mchezaji wa zamani wa Tottenham na Liverpool ambae sasa ni Nahodha wa Republic of Ireland, Robbie Keane.
Baada ya Mechi hii, Man United watasafiri kwenda Miji ya Denver, Washington na Detroit kucheza na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid kwenye Mashindano ya International Champions Cup