Social Icons

Pages

Sunday, 3 November 2013

RONALDO AENDELEA KUONGOZA KATIKA MSIMAMO WA UFUNGAJI WA LA LIGA,


Cristiano Ronaldo amepiga bao mbili na kuiwezesha Real Madrid kuibwaga Rayo Valcano kwa mabao 3-2 pamoja na kuwa ugenini.
Pamoja na ushindi huo, Ronaldo amefikisha mabao 13 na kumpiku  mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa.


Costa ana mabao 12 na hivi karibuni alifunga mawili na kufanikiwa kumpiku Ronaldo.

Lakini mabao mawili ya Ronaldo, yamemuondoa tena Costa kwenye uongozi wa wafungaji.

Kwa kuwa Messi kiwango chake kinaonekana kuyumba, ushindani wa wafungaji katika La Liga unaonekana kuhamia kwa Ronaldo na Costa aliyeamua kuchukua uraia wa Hispania badala ya kwao Brazil.
 
FULU VIWANJA