Social Icons

Pages

Friday, 25 July 2014

FRANK LAMPARD AJIUNGA NEW YORK CITY!



FRANK_LAMPARDKiungo wa zamani wa Chelsea Frank Lampard amejiunga na Klabu itakayocheza Major League Soccer, MLS, huko Marekani New York City FC kwa Mkataba wa Miaka Miwili.
Lampard, mwenye Miaka 36, alimaliza Mkataba wake na Chelsea mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya kuwa Klabuni hapo kwa Miaka 13.
Lampard alihamia Chelsea kutoka West Ham Juni 2001 kwa Uhamisho wa Pauni Milioni 11 na kuweka Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Chelsea kwa kufunga Mabao 211 katika Mechi 649.
New York City FC, ikiwa inamilikiwa na Manchester City, ni Klabu mpya iliyoanzishwa hivi karibuni na itashiriki MLS Mwakani na hivi sasa ndio imeanza kusajili Wachezaji na tayari imeshamnasa Straika wa zamani wa Spain David Villa kutoka Klabu ya Spain Atletico Madrid.
Lakini Villa, mwenye Miaka 32, atacheza kwa Mkopo huko Australia kwenye Klabu ya Ligi A Melbourne City kuanzia Oktoba hadi Desemba na inaaminika Lampard huenda akafuata njia hiyo hiyo.

LAMPARD-Mataji:
-LIGI KUU ENGLAND: 2004-05, 2005-06, 2009-10
-FA Cup: 2006-07, 2008-09, 2009-10, 2011-12
-Ligi Cup: 2004-05, 2006-07
-UEFA Championz Ligi: 2011-12
-Europa Ligi: 2012-13

Hivi sasa Ligi ya MLS inajijenga kwa kuchukua Mastaa mbalimbali kwenye Klabu zao mbalimbali.
Baadhi ya Mastaa hao ni Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Thiery Henry, anaechezea New York Red Bulls, Jermain Defoe, aliekuwa Tottenham, na sasa yuko Toronto FC, Tim Cahill kutoka Everton yuko New York Red Bulls, Obafemi Martins, aliekuwa Newcastle, yupo Seattle Sounders pamoja na Clint Dempsey wakati Robbie Keane, aliewahi kuzichezea Liverpool na Tottenham, yupo LA Galaxy.
Vile vile Staa wa Brazil, Kaka, anatarajiwa kujiunga na Orlando City Mwakani.
 
FULU VIWANJA