Jaja alizaliwa Septemba 21 mwaka 1985 huko Brazili na
kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa mfungaji bora katika timu aliyokuwa
akiichezea ya Itabaina FC iliyopo Kitongoji cha Sergipe.
Yametimia klabu ya soka ya Yanga imempa mkataba wa miaka miwili
mshambuliaji raia wa Brazili Geilson Santana Santos ‘Jaja’ huku Mganda
Hamis Kiiza ‘Diego’akitarajiwa kutupiwa virago ili klabu hiyo ibakiwe na
nyota watano wakigeni kama Sheria za TFF,zinavyoagiza.Jaja aliyekuja Tanzania wiki iliyopita kwa ajili ya majaribio anakuwa mchezajI wa pili kutoka Brazili kusaini Yanga baada ya Andrey Coutinho, kusaini mkataba wa muda kama huo wiki tatu zilizopita.
Katibu Mkuu wa Yanga Beno Njovu aliiambia fulu viwanja Jaja amekuwa na juhudi kubwa kwenye mazoezi ya timu hiyo kiasi cha kumvutia kocha Maximo na kuamua kumpa mkataba huo wa miaka miwili japo hakusema dau ambalo wamemchulia.
“Nikweli Jaja tumempa mkataba wa miaka miwili baada ya kumaliza mazoezi ya asubuhi baada ya kocha Maximo kuridhishwa na kiwango chake,”alisema Njovu.
Jaja alizaliwa Septemba 21 mwaka 1985 huko Brazili na kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa mfungaji bora katika timu aliyokuwa akiichezea ya Itabaina FC iliyopo Kitongoji cha Sergipe nchini Brazili.