Social Icons

Pages

Wednesday, 10 January 2018

SERENGETI YAINGIA MKATABA MWINGINE NA TFF, SASA NI KUDHAMINI LIGI YA WANAWAKE

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)  na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Leo Jumatano Januari 10,2018 wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuidhamini Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kupitia Bia ya Serengeti Lite  mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 450.

''Lukaku aliondoka Everton kufuatia ujumbe wa uchawi''

Mshambuliaji Romelu Lukaku aliamua kuondoka Everton baada ya ujumbe wa ''uchawi'' kumwambia ajiunge na Chelsea kulingana na mwenye hisa mkuu wa klabu ya Everton.
Mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 baadaye alijiunga na Manchester United kwa dau la pauni milioni 75 msimu wa uhamisho uliopita.
Farhad Moshiri aliwaambia wenye hisa katika mkutano na wachezaji kwamba mchezaji huyo alipokea ujumbe ''wa kwenda kuhiji Afrika'' wakati ambapo alitarajiwa kutia saini mkataba mpya katika klabu ya Everton.
Mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea walikuwa wamewasilisha ombi la kutaka kumsajili Lukaku lakini badala yake akajiunga na Manchester United.
''Alikuwa na uchawi na akapokea ujumbe aliotaka kwenda Chelsea'', alisema Moshiri.
Mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea walikuwa wamewasilisha ombi la kutaka kumsajili Lukaku lakini badala yake akajiunga na Manchester United.
Mwezi Machi ajenti wa Lukaku Mino Raiola alikuwa amedai kwamba mkataba mpya wa kusalia Everton ulikuwa umekamilika asilimia 99.9.
''Tulimpatia kandarasi nzuri zaidi ya Chelsea na ajenti wake aliwasili kuja kutia kandarasi'' , Moshiri aliambia mkutano wa kila mwaka wa Everton.
Bilionea huyo wa Iran, Moshiri ambaye alikwa amewekeza dola milioni 150 katika deni la klabu hiyo, alisema kuwa Everton ilimpatia mshambuliaji huyo fedha nyingi ili kusalia.
''Swala la Lukaku halikuwa la kifedha. Iwapo nitaendelea kuwa miliki mkuu wa klabu hiyo maswala ya kifedha hayatakuwa tatizo''.Moshiri alisema kuwa Lukaku baadaye alimpigia simu mamake kabla ya mchezaji huyo kufichua kwamba alipokea ujumbe uliomwambia ajiunge na Chelsea.

Chelsea na Arsenal kukabiliana nusu fainali ya Carabao

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard atashiriki katika mechi dhidi ya Arsenal katika awamu ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la Carabao siku ya Jumatano baada ya kupona jereha.
Mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa pauni milioni 15 kutoka Everton Ross Barkley hatoshiriki kwa kuwa bado anauguza jereha la nyuma ya goti.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ataendelea na marufuku ya kutokalia eneo la wakufunzi uwanjani na badala yake kukaa katika viti vya mashabiki huku kikosi chake kikirudi baada ya kufungwa na klabu ya Nottinham Forest katika kombe la FA.
Granit Xhaka anauguza jeraha la kinena huku Shkodran Mustafi ambaye aligongwa akiwa hajulikani iwapo atashiriki.
  • Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard atashiriki mechi hiyo
Mfumo wa kiteknolojia wa video ya kumsaidia refa VAR utatumika katika awamu zote mbili za nusu fainali hiyo.
Arsenal haijashinda kombe hilo kwa kipindi cha miaka 25 huku Chelsea ikiweza kushinda mara ya mwisho 2015.

Antonio Conte: Sitasahau mzozo wangu na Mourinho

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema 'hatausahau' mzozo ambao alikuwa nao na meneja wa Manchester United, Jose Mourinho akiongeza kwamba hiyo ni shida miongoni mwao hao wawili na sio kwa klabu hizo.
Mourinho aliendelea kumtupia Conte maneno siku ya Jumamosi kwa kusema yeye hawezi "kupigwa marufuku yoyote kwa kosa la kupanga matokeo ya mechi", ambapo awali alikuwa amezungumzia kuhusu "mchekeshaji" uwanjani.
Mwitaliano huyo alijibu matamshi ya Mourinho kwa kumuita mtu ''mdogo.''
"Alitumia maneno makali,'' Conte aliongeza kwenye mkutano wake na wanahabari siku ya Junanne.
''Sitasahau hili.''
Antonio Conte
Conte amesema hajutii kusema ''Huyu ni mtu mdogo'' kwenye matamshi yake na hakuna sababu yoyote kwa Chama cha Mameneja wa Ligi ya Premia kuingilia kati.
"Hii si shida kutoka kwa klabu, ni shida kati yetu sisi. Nimenyamaza,'' aliongeza.

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA KAPERA

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Omary Kapera aliyefariki dunia juzi kuzikwa jana mchana.
Image result for wallace karia

Rais Karia amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo; "Nimeshtushwa na taarifa hizo za kifo cha Kapera hasa ikichukuliwa bado tupo kwenye majonzi ya kumpoteza mchezaji mwingine wa zamani Athuman Juma Chama, kwa niaba ya Shirikisho natoa pole kwa wote walioguswa na msiba huo kuanzia kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki,”alisema Rais Karia.

Omar Kapera ‘Mwamba Kifua’ alikuwa sentahafu wa Yanga tangu miaka ya 1960 hadi 1977 alipokwenda kujiunga na Nyota Afrika ya Morogoro kufuatia mgogoro mkubwa uliobuka klabu ya Jangwani mwaka 1976.

Kapera na kundi la wachezaji wenzake walioondoka Yanga baada ya mgogoro huo wa kihistoria, baadaye walirejea Dar es Salaam kuasisi Pan Africans iliyokuja kuwa tishio pia katika soka ya Tanzania kabla ya kupoteza makali baada ya muongo mmoja.


Kapera alikuwepo kwenye kikosi cha Yanga kilichoichapa Simba SC 5-0 Juni 1, mwaka 1968 Uwanja wa Karume, Dar es Salaam siku hiyo mabao ya wana Jangwani yakifungwa na Maulid Dilunga mawili dakika ya 18 kwa penalti na 43, Salehe Zimbwe dakika za 54 na 89 na Kitwana Manara ‘Popat’ dakika ya 86.
Na ni kikosi hicho kilichofika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili mfululizo mwaka 1969 na 1970 na kutolewa na Asante Kotoko ya Ghana mara zote.

Friday, 5 January 2018

ALICHOSEMA KOCHA WA SIMBA KUHUSIANA NA BOCCO KUWA NAHODHA MKUU

Ukisema kuwa amewanyamazisha pia ni sawa maana Joh Raphael Bocco amekuwa akionyesha kiwango bora dhidi ya wale waliokuwa wakiamini kuwa hana msaada.
Image result for MASOUD DJUMA SIMBA CLUB

Kiwango anachoendelea kukionyesha mshambuliaji, John Bocco kimetosha kwa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Mrundi, Masoud Djuma kumpa unahodha mkuu nyota huyo.

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu mshambuliaji huyo aifungie mabao muhimu katika mechi dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na matokeo kumalizika kwa Simba kushinda mabao 2-0.

Bocco anapewa cheo hicho cha nahodha mkuu akimrithi beki Mzimbabwe, Method Mwanjali aliyesitishiwa mkataba wake katika usajili wa dirisha dogo ambalo lilifungwa Desemba 15, mwaka huu.

Djuma alisema awali kabla ya kumpa cheo hicho, alikuwa ni nahodha msaidizi wa timu hiyo akisaidiana na beki wa kushoto, Hussein Mohamed ‘Zimbwe Jr’.

Djuma alisema anafurahishwa na kiwango cha Bocco anayecheza vizuri kwa kufuata maelekezo yake ambayo anampa kabla na baada ya mechi katika kuhakikisha anatimiza majukumu ya kufunga mabao.

“Nimempa cheo hicho cha unahodha mkuu kutokana na nidhamu yake ya ndani na nje ya uwanja, pia jinsi anavyotimiza majukumu yake akiwa uwanjani kwa maana kufunga mabao na kiwango kizuri anachokionyesha,” alisema Djuma.

Mohamed Salah atawazwa mchezaji bora wa CAF Afrika mwaka 2017

Nyota wa timu ya Liverpool ambaye ni raia wa Misri, Mohamed Salah ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka 2017 Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Salah alikuwa akishindana na Pierre-Emerick Aubameyang, na Sadio Mane na akaibuka bora zaidi kwa wingi wa kura na ubora awapo kiwanjani.
 Mohamed Salah
Mane na Salah walihudhuria sherehe za kutangazwa kwa washindi mjini Accra, Ghana saa 24 kabla ya mechi ya Kombe la FA Ijumaa ambapo klabu yao ya Liverpool itacheza dhidi ya Everton.
Salah hataweza kucheza mechi hiyo kwani ameumia.

Salah ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza maishani mwake.
Salah alionekana kuitetea vyema timu yake ya Liverpool mwaka 2017 baada ya kujipatia goli 23 katika mechi 29 baada ya kujiunga katika ligi kuu ya England akitokea timu ya AS Roma.

Serena Williams ajiondoa kutoka kwa Australian Open 2018

Mchezaji nyota wa tenisi duniani Serena Williams amejiondoa kutoka kwa michuano ya mwezi huu ya Australian Open mjini Melbourne.
 Serena Williams in action in Abu Dhabi
Mmarekani huyo wa miaka 36 alicheza mechi yake ya kwanza wiki iliyopita tangu ajifungue Septemba.

Williams, ambaye ameshinda Grand Slam mara 23 na ndiye bingwa mtetezi wa Australian Open alisema: "Ingawa nakaribia sana, sijafika pahali ninapotaka."

Alhamisi, Mwingereza Andy Murray pia alijiondoa kutoka kwa michuano hiyo itakayoanza 15 Januari.

William alikuwa na ujauzito wa wiki sita wa binti yake Olympia aliposhinda taji lake la saba la Australian Open mwaka 2017.
Serena Williams ambaye kwa sasa ameorodheshwa nambari 22 duniani alisema: "Mkufunzi wangu na maafisa wangu husema mara kwa mara kwamba unafaa kwenda kwa mashindano iwapo uko tayari kushindana hadi mwisho

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 05.01.2018

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Liverpool watamruhusu Philippe Coutinho, 25, kuhamia Barcelona mwezi huu wa Januari kwa £140m. (Times)

Chelsea wanamtaka meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone achukue nafasi ya Antonio Conte katika klabu hiyo mwisho wa msimu. (Times )

Chelsea wamezidisha juhudi zao za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Everton na England Ross Barkley, 24, na pia wameulizia kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa England na West Ham Andy Carroll, 28. (Mail)

Mchezaji wa Celtic na Scotland Kieran Tierney, 20, amejumuishwa katika orodha ya mabeki wa kushoto ambao Manchester United wanawatafuta kuimarisha safu yao ya ulinzi, pamoja na kinda wa Fulham Ryan Sessegnon, 17. (Daily Record)

Paris St Germain wanatarajiwa kutoa ushindani kwa Tottenham katika kutafuta saini ya Sessegnon ambaye thamani yake imekadiriwa kuwa £30m. (Mirror)

Juventus wana imani kwamba watafanikiwa kumchukua Emre Can kutoka Liverpool bila kulipa ada yoyote mwisho wa msimu.

Klabu hiyo ya Serie A imemuahidi mchezaji huyo wa miaka 23 mshahara wa £85,000 kwa wiki. (Guardian)

Manchester United wameanzisha mazungumzo ya kuongeza mikataba ya wachezaji wane kwa mwaka mmoja. Wachezaji hao ni viungo wa kati wa Uhispania Juan Mata, 29, na Ander Herrera, 28, beki wa England Ashley Young, 32, na beki Mholanzi Daley Blind, 27. (Mirror)

Manchester United wanataka sana kumnunua beki wa kushoto wa Juventus Sandro lakini wanavunjwa moyo na Juve kutotaka kumuuza mchezaji huyo wa miaka 26. (Express)

Tottenham wanatarajiwa kutoa mikataba mipya yenye donge nono zaidi kwa mshambuliaji wa England Harry Kane, 24, na beki wa Ubelgiji Toby Alderweireld, 28. (Independent)

Marseille wanamnyatia kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere lakini mchezaji huyo wa miaka 26 anataka kusalia na Gunners. (Mail)

Mkufunzi mkuu wa Monaco Leonardo Jardim amesema hana nia ya kumuuza mshambuliaji wake Mfaransa Thomas Lemar, 22, kwa Liverpool mwezi huu. (Liverpool Echo)

Meneja wa Paris St-Germain Unai Emery amefungua mlango kwa winga wa Brazil Lucas Moura, 25, na mwenzake wa Ufaransa Hatem Ben Arfa, 30, kuihama klabu hiyo Januari. (L'Equipe)

Mbelgiji Thibaut Courtois, 25, anakaribia kutia saini mkataba mpya Chelsea baada ya klabu hiyo kumpa ujira wa zaidi ya £200,000 kwa wiki, hatua itakayomfanya kuwa kipa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Telegraph)

Beki wa Chelsea David Luiz, 30, anataka sana kuondoka klabu hiyo na anatumaini Real Madrid watamtaka. (Mundo Deportivo - kupitia Express)

Mkufunzi mkuu wa Newcastle Rafa Benitez anatafakari uwezekano wa kutaka kumnunua nahodha wa Watford Troy Deeney, 29. (Northern Echo)

Newcastle na Burnley nao wanataka kumnunua kiungo wa kati Mhispania Jonathan Viera, 28, kutoka Las Palmas. (Telegraph)

Sunderland wanakaribia kumchukua mshambuliaji mchanga wa Liverpool Ben Woodburn mwenye miaka 18 kwa mkopo. (Star)

Everton wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Nice na Ivory Coast Jean Michael Seri, 26. (Sky Sports)

Meneja wa Everton Sam Allardyce hataki kumwachilia mshambuliaji Sandro Ramirez, 22, atoke nje kwa mkono Januari lakini anasema hana usemi wowote kuhusu hilo. (Liverpool Echo)
Crystal Palace wamewasilisha ofay a kutaka kumnunua beki wa kati wa Lille Ibrahim Amadou, 24. (Sun)

Besiktas wanataka kumnunua mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 29. (Leicester Mercury)

Islam Slimani alipokuwa Sporting Lisbon


Barcelona nao wanakaribia kumchukua beki wa kati wa Palmeiras ambaye ni raia wa Colombia Yerry Mina, 23. (Marca)

Manchester City nao wamesalia makini sana kutafuta walinzi sokoni kutokana na mahitaji ya kuwa katika michuano mingi. (Manchester Evening News)

Tamko la Bayern Munich kuhusu kiungo wa kati wa Schalke Leon Goretzka limekera klabu hiyo, na kuimarisha nafasi ya Liverpool kumnunua mchezaji huyo wa miaka 22. (Star)

Meneja wa zamani wa Bundesliga Jos Luhukay ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Carlos Carvalhal klabu ya Sheffield Wednesday. (Yorkshire Post)
 
FULU VIWANJA