Mchezaji nyota wa tenisi duniani Serena Williams amejiondoa kutoka kwa michuano ya mwezi huu ya Australian Open mjini Melbourne.

Williams, ambaye ameshinda Grand Slam mara 23 na ndiye bingwa mtetezi wa Australian Open alisema: "Ingawa nakaribia sana, sijafika pahali ninapotaka."
Alhamisi, Mwingereza Andy Murray pia alijiondoa kutoka kwa michuano hiyo itakayoanza 15 Januari.
William alikuwa na ujauzito wa wiki sita wa binti yake Olympia aliposhinda taji lake la saba la Australian Open mwaka 2017.
Serena Williams ambaye kwa sasa ameorodheshwa nambari 22 duniani alisema: "Mkufunzi wangu na maafisa wangu husema mara kwa mara kwamba unafaa kwenda kwa mashindano iwapo uko tayari kushindana hadi mwisho