Nyota wa timu ya Liverpool ambaye ni
raia wa Misri, Mohamed Salah ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji
bora wa Afrika wa mwaka 2017 Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Mane na Salah walihudhuria sherehe za kutangazwa kwa washindi mjini Accra, Ghana saa 24 kabla ya mechi ya Kombe la FA Ijumaa ambapo klabu yao ya Liverpool itacheza dhidi ya Everton.
Salah hataweza kucheza mechi hiyo kwani ameumia.
Salah ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza maishani mwake.
Salah alionekana kuitetea vyema timu yake ya Liverpool mwaka 2017 baada ya kujipatia goli 23 katika mechi 29 baada ya kujiunga katika ligi kuu ya England akitokea timu ya AS Roma.