Kuna uwezekano mkubwa kwamba
Liverpool watamruhusu Philippe Coutinho, 25, kuhamia Barcelona mwezi huu
wa Januari kwa £140m. (Times)
Chelsea wanamtaka meneja wa
Atletico Madrid Diego Simeone achukue nafasi ya Antonio Conte katika
klabu hiyo mwisho wa msimu. (Times )
Chelsea wamezidisha juhudi
zao za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Everton na England Ross
Barkley, 24, na pia wameulizia kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji
wa England na West Ham Andy Carroll, 28. (Mail)
Mchezaji wa Celtic na Scotland Kieran Tierney, 20, amejumuishwa
katika orodha ya mabeki wa kushoto ambao Manchester United wanawatafuta
kuimarisha safu yao ya ulinzi, pamoja na kinda wa Fulham Ryan Sessegnon,
17. (Daily Record)
Paris St Germain wanatarajiwa kutoa ushindani
kwa Tottenham katika kutafuta saini ya Sessegnon ambaye thamani yake
imekadiriwa kuwa £30m. (Mirror)
Juventus wana imani kwamba watafanikiwa kumchukua Emre Can kutoka Liverpool bila kulipa ada yoyote mwisho wa msimu.
Klabu hiyo ya Serie A imemuahidi mchezaji huyo wa miaka 23 mshahara wa £85,000 kwa wiki. (Guardian)
Manchester
United wameanzisha mazungumzo ya kuongeza mikataba ya wachezaji wane
kwa mwaka mmoja. Wachezaji hao ni viungo wa kati wa Uhispania Juan Mata,
29, na Ander Herrera, 28, beki wa England Ashley Young, 32, na beki
Mholanzi Daley Blind, 27. (Mirror)
Manchester United wanataka sana
kumnunua beki wa kushoto wa Juventus Sandro lakini wanavunjwa moyo na
Juve kutotaka kumuuza mchezaji huyo wa miaka 26. (Express)
Tottenham
wanatarajiwa kutoa mikataba mipya yenye donge nono zaidi kwa
mshambuliaji wa England Harry Kane, 24, na beki wa Ubelgiji Toby
Alderweireld, 28. (Independent)
Marseille wanamnyatia kiungo wa
kati wa Arsenal Jack Wilshere lakini mchezaji huyo wa miaka 26 anataka
kusalia na Gunners. (Mail)
Mkufunzi mkuu wa Monaco Leonardo Jardim amesema hana
nia ya kumuuza mshambuliaji wake Mfaransa Thomas Lemar, 22, kwa
Liverpool mwezi huu. (Liverpool Echo)
Meneja wa Paris St-Germain
Unai Emery amefungua mlango kwa winga wa Brazil Lucas Moura, 25, na
mwenzake wa Ufaransa Hatem Ben Arfa, 30, kuihama klabu hiyo Januari.
(L'Equipe)
Mbelgiji Thibaut Courtois, 25, anakaribia kutia saini mkataba
mpya Chelsea baada ya klabu hiyo kumpa ujira wa zaidi ya £200,000 kwa
wiki, hatua itakayomfanya kuwa kipa anayelipwa pesa nyingi zaidi
duniani. (Telegraph)
Beki wa Chelsea David Luiz, 30, anataka sana
kuondoka klabu hiyo na anatumaini Real Madrid watamtaka. (Mundo
Deportivo - kupitia Express)
Mkufunzi mkuu wa Newcastle Rafa
Benitez anatafakari uwezekano wa kutaka kumnunua nahodha wa Watford Troy
Deeney, 29. (Northern Echo)
Newcastle na Burnley nao wanataka kumnunua kiungo wa kati Mhispania Jonathan Viera, 28, kutoka Las Palmas. (Telegraph)
Sunderland wanakaribia kumchukua mshambuliaji mchanga wa Liverpool Ben Woodburn mwenye miaka 18 kwa mkopo. (Star)
Everton wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Nice na Ivory Coast Jean Michael Seri, 26. (Sky Sports)
Meneja
wa Everton Sam Allardyce hataki kumwachilia mshambuliaji Sandro
Ramirez, 22, atoke nje kwa mkono Januari lakini anasema hana usemi
wowote kuhusu hilo. (Liverpool Echo)
Crystal Palace wamewasilisha ofay a kutaka kumnunua beki wa kati wa Lille Ibrahim Amadou, 24. (Sun)
Besiktas wanataka kumnunua mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 29. (Leicester Mercury)
Barcelona nao wanakaribia kumchukua beki wa kati wa Palmeiras ambaye ni raia wa Colombia Yerry Mina, 23. (Marca)
Manchester
City nao wamesalia makini sana kutafuta walinzi sokoni kutokana na
mahitaji ya kuwa katika michuano mingi. (Manchester Evening News)
Tamko la Bayern Munich kuhusu kiungo wa kati wa Schalke Leon
Goretzka limekera klabu hiyo, na kuimarisha nafasi ya Liverpool kumnunua
mchezaji huyo wa miaka 22. (Star)
Meneja wa zamani wa Bundesliga
Jos Luhukay ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi iliyoachwa
wazi na Carlos Carvalhal klabu ya Sheffield Wednesday. (Yorkshire Post)