Ukisema
kuwa amewanyamazisha pia ni sawa maana Joh Raphael Bocco amekuwa
akionyesha kiwango bora dhidi ya wale waliokuwa wakiamini kuwa hana
msaada.

Kiwango
anachoendelea kukionyesha mshambuliaji, John Bocco kimetosha kwa Kaimu
Kocha Mkuu wa Simba Mrundi, Masoud Djuma kumpa unahodha mkuu nyota huyo.
Hiyo,
ikiwa ni siku chache tangu mshambuliaji huyo aifungie mabao muhimu
katika mechi dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa wikiendi iliyopita kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na matokeo kumalizika kwa Simba
kushinda mabao 2-0.
Bocco
anapewa cheo hicho cha nahodha mkuu akimrithi beki Mzimbabwe, Method
Mwanjali aliyesitishiwa mkataba wake katika usajili wa dirisha dogo
ambalo lilifungwa Desemba 15, mwaka huu.
Djuma
alisema awali kabla ya kumpa cheo hicho, alikuwa ni nahodha msaidizi wa
timu hiyo akisaidiana na beki wa kushoto, Hussein Mohamed ‘Zimbwe Jr’.
Djuma
alisema anafurahishwa na kiwango cha Bocco anayecheza vizuri kwa
kufuata maelekezo yake ambayo anampa kabla na baada ya mechi katika
kuhakikisha anatimiza majukumu ya kufunga mabao.
“Nimempa
cheo hicho cha unahodha mkuu kutokana na nidhamu yake ya ndani na nje
ya uwanja, pia jinsi anavyotimiza majukumu yake akiwa uwanjani kwa maana
kufunga mabao na kiwango kizuri anachokionyesha,” alisema Djuma.