Social Icons

Pages

Sunday, 9 August 2015

WENGER AKATAA KUMLAUMU KIPA CECH KWA KIPIGO CHAO CHA NYUMBANI!


Huku Wachambuzi wakimnyooshea kidole Kipa mpya wa Arsenal Petr Cech kwa kufanya makossa yaliyoruhusa Bao zote walipopigwa 2-0 Leo kwao Emirates na West Ham katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu mpya, Meneja Arsene Wenger amekataa kumshushia lawama Kipa huyo.Arsenal manager Arsene Wenger, right, puts his hand to his head during the English Premier League  soccer match against West Ham United  at the Emirates Stadium, London Sunday Aug. 9, 2015.  Arsenal lost their first match of the new season 2-0.(Andrew Matthews/PA via AP) UNITED KINGDOM OUT
Cech, alienunuliwa kutoka Chelsea, aliutokea Mpira wa Frikiki ili aupanchi lakini akaukosa na kutoa mwanya kwa Cheikhou Kouyate kufunga kilaini kwa Kichwa Bao la kwanza na kisha shuti la mbali la Mauro Zarate kumhadaa Cech kwenye Posti yake ya karibu na kutinga.Cech: Mistakes weren't in the script
Lakini Wenger, akiongea mara baada ya kipigo hicho, ameeleza: “Ni kutokuwa makini kwa pamoja. Kuna vitu vingi hapo. Nilijua kama ile frikiki itapigwa vizuri basi tutakuwa mashakani kutokana na tulivyojipanga, tulijiua wenyewe. Sijaongea na Cech lakini sikuona Mchezaji mwingine yeyote akicheza kwa kufurahisha hii Leo hivyo ni ngumu kumlaumu mmoja.”
Aliongeza: “Pasi zetu hazikuwa nzuri. Leo lazima tujitazame wenyewe. Hatukuwa wazuri.”Arsenal manager Arsene Wenger looks on as Alexis Sanchez waits to come on as substitute
Mara baada ya Wikiendi iliyopita kuwafunga Mabingwa Chelsea Bao 1-0 huko Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii, Wachambuzi wengi huko England waliipa nafasi kubwa Arsenal kuwemo rasmi kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa Msimu huu lakini kichapo hiki cha Leo kimeleta fikra nyingine.Cech: Nightmare Arsenal debut was not in the script

 
FULU VIWANJA