Straika wa Brazil anaechezea Klabu ya Barcelona Neymar anaugua Ugonjwa uitwao ‘matumbwimatumbwi’ na atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 2 na hivyo kuzikosa Mechi za mwanzo kabisa za Msimu mpya.
Mechi atakazozikosa Kepteni huyo wa Brazil ni ile ya kugombea UEFA Super Cup itakayochezwa huko Tblisi, Georgia Jumanne ijayo dhidi ya Seville na Mechi mbili za kuwania Spanish Super Cup dhidi ya Athletic Bilbao hapo Agosti 14 na 17.
Pia huenda akaikosa Mechi ya kwanza kabisa ya La Liga Ugenini na Athletic Bilbao hapo Agosti 23.
Msimu uliopita, Neymar, mwenye Miaka 23, aliifungia Barcelona Magoli 39 wakati ilipotwaa Trebo yaani Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na UEFA CHAMPIONZ LIGI.