Mzinga wa mbali wa Mbrazil Philippe Coutinho katika Dakika ya 86 Leo umewapa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Wenyeji Stoke City katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu huko Britannia Stadium, Uwanja ambao walipigwa 6-1 na Stoke City katika Mechi yao ya mwisho kabisa ya Ligi Kuu England Msimu uliopita.

Ukiondoa kosakosa za Timu ya Stoke kupitia Beki wao Glen Johnson, Mchezaji wa zamani wa Liverpool, na pale Frikiki ya Charlie Adam, Mchezaji mwingine wa zamani wa Liverpool, ilipookolewa na Kipa Simon Mignolet, Mechi hii ilipooza kwa sehemu kubwa.
