Wachezaji wa tano wa tennis (lawn)
wa Tanzania watakao iwakilisha nchi
katika michuano michuano ya vijana
ya ITF ya Afrika itakayofanyika
Tunisia kuanzia Machi 9 mpaka
Kwa mujibu wa viongozi wa chama
cha tennis Tanzania (TTA), ushiriki
wao utaleta tija katika maendeleo ya
mchezo huo nchini.
Tennisi ni moja ya michezo
inayokuwa kwa kasi nchini Tanzania
na chama cha mchezo huo
kimefanikiwa kuwa wenyeji waq
michuano mbalimbali ikiwemo ya
Afrika ya Mashariki na Kati
inayojumuisha nchi mbalimbali za
Afrika.
Kwa mujibu wa kocha Majuto
Majaliwa, miongoni mwa wachezaji
watakaoiwakilisha nchi ni Georgina
Kaindoah (yupo Afrika ya Kusini
kimasomo na mazoezi) , Emmanuel
Mallya, Frank Mernad, Deogratius
Ernest na Mandi Furaji (yupo
Uingereza kimasomo na mazoezi-.
Michuano hiyon itafanyika katika mji
wa Tunis. Nchi mbalimbali za Afrika
zitashiriki na kuwakilishwa na
wachezaji watano.
Miongoni mwa nchi ambazo tayari
zimetaja wachezaji wake ni pamoja
na Rwanda, ambapo kwa mujibu wa
vyombo vya habari, waliochaguliwa
kuiwakilisha nchi hiyo ni Ernest
Habiyambere, Cedric Tuyishimwe,
Mutuyimana Chantal, Flavia Kayitesi
na Evelyne Kwizera, ambao walifuzu
katika michuano iliyofanyika Dar es
Salaam, Tanzanua kati ya Januari
10-19.