Social Icons

Pages

Monday, 2 February 2015

Francis Cheka : miaka mitatu jel

Bondia wa kulipwa nchini Tanzania,
Francis Cheka, ambaye ni maarufu
kwa jina la SMG, amehukumiwa
kifungo cha miaka mitatu jela na
faini ya Sh milioni moja kwa kosa la
kumpiga meneja waje wa baa yake ,
Bahati Kibanda.

Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka
jana kwa kumpiga na kumsababishia
maumivu makali Kibanda ambaye
alikwenda hapo kudai fedha zake
katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi
ijulikanayo kwa jina la Vijana Social
Hall.

Cheka anayeshikilia mkanda wa WBF
alipandishwa Kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa
wa Morogoro, kwa shitaka hilo
lililosomeka kuwa ni la shambulio la
kudhuru mwili na kujeruhi.
Hakimu Mwandamizi wa mahakama
ya mkoa wa Morogoro Said Msuya
alikubaliana na ushahidi uliotolewa
na upande wa mashtaka na
kuthibitisha shitaka hilo.

Cheka anadaiwa kutenda kosa hilo
kwa Kabanda ambaye alikuwa ni
Meneja wa baa yake ya Vijana Social
iliyopo maeneo ya Sabasaba katika
Manispaa ya Morogoro baada ya
kudaiwa kutoridhishwa na mahesabu
ya mauzo.

Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu
hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na
watu wengine wanaotumia vibaya
nguvu zao kwa watu wengine na
anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia
ya Sh milioni moja.

Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya
kujitetea, bondia huyo hakutoa
maelezo yoyote na kuiachia
mahakama hiyo kutoa adhabu
inayostahili kwa bondia huyo
aliyejizolea sifa kemkem katika
ngumi za kulipwa nchini.
Hata hivyo, familia ya Cheka
inampango wa kukata rufaa kupinga
hukumu hiyo.

 
FULU VIWANJA