YANGA hii Leo wakiwa huko
Sokoine Jijini Mbeya
wamechukua usukani wa Ligi
Kuu Vodacom baada ya
kuitandika Tanzania Prisons
Bao 3 - 0 wakati waliokuwa
Vinara , Azam FC , ambao pia
ndio Mabingwa Watetezi ,
kutoka Sare 0- 0 na Ruvu
Shooting huko Mabatini ,
Mlandizi , Mkoa wa Pwani.
Yanga sasa wapo kileleni
wakiwa Pointi 2 mbele ya
Azam FC huku Timu hizo
zikiwa zote zimecheza Mechi
14 kila mmoja .
Bao za Yanga zilifungwa na
Simon Msuva, Bao 2 , na
Mbrazil Coutinho aliepiga Bao
1 lakini yeye ndie Nyota wa
Gemu baada ya kutengenezai
Bao zote 2 za Msuva
alieunganisha Kona zake mbili
Dakika za 3 na 62 .
Bao la Coutinho lilifungwa
Dakika ya 11 na kusindikizwa
wavuni na Beki wa Prisons
katika harakati za kuokoa
lakini Bao hilo linabaki kwa
Mbrazil huyo kwa vile Mpira
huo hata kama Beki huyo
asingeugusa ulikuwa unatinga
tu.
Hizi Mechi za Leo ni za viporo
kwa Yanga na Azam Fcn na
wote watatinga tena dimbani
Jumapili kwa Yanga kubaki
huko huko Sokoine Mbeya
kucheza na Mbeya City na
Azam FC kuwa kwao Azam
Complex , Chamazi , kwenye
Viunga vya Jiji la Dar es
Salaam kucheza na Tanzania
Prisons.
Jumapili hiyo hiyo ipo Mechi
moja zaidi huko Kambarage,
Mjini Shinyanga , wakati Stand
United itakapoikaribisha
Simba.
Lakini kabla ya hiyo Jumapili ,
Jumamosi zipo Mechi 3 za Ligi
huko Miji ya Shinyanga ,
Mtwara na Tanga.