Hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la
Mabingwa barani Ulaya UEFA Champions’
League imeanza hapo jana kwa kuzalisha sare
mbili katika viwanja viwili tofauti.
Katika dimba la Parc des Princes nchini
Ufaransa Chelsea imetoshana nguvu na
PSG kwa kutoka sare ya bao 1-1.
Chelsea walikuwa wa Kwanza kupata bao
kupitia kwa Branislav Ivanovic dakika ya
36 lakini kipindi cha Pili kupitia kwa
Edinson Cavan PSG walisawazisha ikiwa
ni dakika ya 54.
Mechi ya marudiano itapigwa Machi 11
katika dimba la Stamford Bridge, ambapo
Chelsea italazimika kupata ushindi wa
aina yoyote, au suluhu ya bila kufungana.
Katika mchezo mwingine Bayern Munich
ya Ujerumani imeshindwa kutamba
nyumbani kwa Shakhtar Donetsk Arena
Lviv nchini Urusi kwa kulazimishwa
suluhu ya bila kufungana.
Katika mchezo huu Bayern wamelazimika
kucheza pungufu kuanzia dakika ya 65
baada ya kiungo wao Xabi Alonso kutolewa
nje kwa kadi nyekundu.
Mchezo wa marudiano utafanyika Fußball
Arena München Machi 11, 2015 ambapo
Bayern italazimika kushinda ili kuingia
Robo Fainali.