Social Icons

Pages

Monday, 2 February 2015

LA LIGA: MESSI APIGA BAO LA USHINDI BARCA , IPO 1 NYUMA YA REAL!

Lionel Messi alifunga Bao la
ushindi Jana Uwanjani Nou
Camp wakati Barcelona inatoka
mara mbili nyuma na kuifunga
Villareal Bao 3 - 2 katika Mechi
ya La Liga .

Sasa Barca wako Pointi 1
nyuma ya Vinara Real Madrid
lakini Barcelona wamecheza
Mechi 1 zaidi.

Barca walijikuta wako nyuma
kwa Bao la Dakika ya 30 la
Denis Cheryshev lakini Neymar
akarudisha Dakika ya 45 na
Luciano Vietto kuwapeleka
Villareal mbele kwa mara ya
Pili kwa Bao la Dakika 51

Kisha Rafinha Alacantara
akaisawazishia Barca Dakika
ya 53 na Lionel Messi kupiga
Bao la ushindi katika Dakika ya
55.l

 
FULU VIWANJA