MAJUZI, utata uligubika Mechi
ya Wenyeji Equatorial Guinea
kwenye Robo Fainali ya Kombe
la Mataifa ya Afrika wakati
Refa kutoka Mauritius
Seechurn Rajindaparsad
alipoikatili Tunisia kutinga
Nusu Fainali baada ya kuwapa
Wenyeji Penati ya Dakika za
Majeruhi na kusawazisha.
Katika Mechi hiyo , Refa
Rajindaparsad aliipa Penati
Equatorial Guinea na kupigwa
na kufungwa na Javier Balboa
na Gemu kulazimika kwenda
Dakika za Nyongeza 30
ambapo Javier Balboa alipiga
Bao la Pili na Equatorial Guinea
kuilaza Tunisia 2- 1 .
Akiongea baada ya Mechi hiyo,
Meneja wa Tunisia, Georges
Leekens , Raia wa Belgium,
alilalamika: “Nataka
Wanahabari wote waliokuwepo
waonyeshe picha za tukio lile
ili Dunia iamue kama ile
ilikuwa Penati kweli au la!”
Aliongeza: “ Katika Miaka
yangu 45 kwenye Soka [15
kama Mchezaji na 30 kama
Kocha] sijaona kitu kama kile.
Ni uamuzi mbovu. Ni ngumu
kukubali uonevu kama ule ! Sio
jambo jema kwa Soka !
Mwaka 2011 , huko Morocco ,
Mashabiki wa Soka
walianzisha Tovuti maalum
iliyoitwa ‘Wamorocco Milioni 1
dhidi ya Refa Seechurn
Rajindraparsad. ’ kulalamika
uchezeshaji wa Refa huyo
kwenye Mechi ya Mchujo ya
Kombe la Afrika iliyochezwa
huko Annaba Nchini Algeria
kati ya Algeria na Morocco.
Kwenye Mechi hiyo Morocco
walilalamikia Penati dhidi yao
pamoja na kuchezewa Rafu
mbaya bila Refa Seechurn
Rajindraparsad kujali.
Mchezaji wa Morocco ambae
sasa huchezea Crystal Palace,
Marouane Chamakh , wakati
huo alilalama: “ Ilikuwaje
wamuweke Refa huyu ?
Alivuruga kila kitu!”
Wachezaji wa Morocco , kama
walivyofanya wa Tunisia hivi
Juzi, walimsakama Refa
Seechurn Rajindraparsad na
hakuna Mchezaji aliewekwa
kibano .
Refa Seechurn Rajindraparsad,
mwenye Miaka 44 , hivi sasa
anachezesha Fainali za Kombe
ya Mataifa ya Afrika kwa mara
ya 4 na ameshachezesha
Mechi kubwa Barani Afrika
zaidi ya 80 zikiwemo Mechi za
Mchujo za Kombe la Dunia.
AFCON 2015