Social Icons

Pages

Saturday, 31 January 2015

EMMANUEL OKWI YUPO FITI KUIVAA JKT RUVU

KIUNGO mshambuliaji wa Simba Sc,
Mganda Emmanuel Anord Okwi
anatarajia kuivaa JKT Ruvu leo
uwanja wa Taifa katika mechi ya ligi
kuu Tanzania bara.

Afisa habari wa Simba, Humphrey
Nyasio amezungumza na mtandao huu
dakika chache zilizopita akiwa uwanja
wa mazoezi wa JKT Mbweni ambapo
Simba inaendelea na mazoezi hivi
tunavyoongea na kueleza kuwa Okwi
yuko fiti na atacheza mechi ya kesho.

“Nipo hapa uwanjani JKT Mbweni,
Okwi anaendelea na mazoezi. Kesho
atacheza”. Amesema Nyasio.
Pia Nyasio amesema beki wa pembeni
Hassan Ramadhan Kessy yuko fiti
kucheza kesho na muda huu
unaendelea na mazoezi.

Hata hivyo, Afisa habari huyo
amesema Simba itaendelea kuikosa
huduma ya kiungo Said Hamis Ndemla
ambaye bado anasumbuliwa na
majeruhi.

Okwi, Ndemla na Kessy waliikosa
mechi ya jumatano iliyopita uwanja
wa Taifa ambapo Mnyama Simba
alichapwa 2-1 na Mbeya City.

Nyasio amesema kesho watapambana
kupata ushindi, licha ya kukiri kuwepo
kwa changamoto katika michuano ya
ligi kuu.

 
FULU VIWANJA