Social Icons

Pages

Monday, 2 February 2015

TFF MBIONI KUPATA MDHAMINI FDL


Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania ( TFF) liko mbioni
kupata mdhamini wa Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) .

Tunatarajia mdhamini huyo
atakuwa tayari kwa ajili ya
msimu wa 2015 /2016 .
Ligi Daraja la Kwanza
inashirikisha timu 24
zinazocheza katika makundi
mawili ya timu 12 kila moja
kwa mtindo wa nyumbani na
ugenini .

Timu zinazocheza FDL msimu
huu ni African Lyon (Dar es
Salaam) , African Sports
(Tanga ), Ashanti United (Dar es
Salaam) , Burkina Faso
(Morogoro ), Friends Rangers
(Dar es Salaam) , Geita Gold
(Geita ) , Green Warriors (Dar es
Salaam) , JKT Kanembwa
(Kigoma) , JKT Mlale ( Ruvuma)
na JKT Oljoro (Arusha ).
Nyingine ni Kimondo ( Mbeya) ,
Kinondoni Municipal Council
(Dar es Salaam) , Kurugenzi
(Iringa ), Lipuli (Iringa) ,
Majimaji ( Ruvuma), Mwadui
(Shinyanga ) , Panone FC
(Kilimanjaro ), Polisi Dar es
Salaam, Polisi Dodoma, Polisi
Mara , Polisi Tabora , Rhino
Rangers (Tabora ), Toto
Africans (Mwanza ), na Villa
Squad (Dar es Salaam).
KIPA BORA WANAWAKE
AZAWADIWA 500 ,000 / -
Kipa bora wa michuano ya
Kombe la Taifa la Wanawake ,
Belina Julius wa Temeke
amezawadiwa sh. 500 ,000 na
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk
Fenella Mukangara .

Dk Mukangara alitoa zawadi
hiyo baada ya mechi ya fainali
ya michuano iliyomalizika jana
kwenye Uwanja wa Azam
Complex uliopo Chamazi jijini
Dar es Salaam. Dk Mukangara
alikuwa mgeni rasmi kwenye
fainali hiyo.

Temeke ndiyo walioibuka
mabingwa wa michuano hiyo
iliyofanyika kwa mara ya
kwanza nchini baada ya
kuilaza Pwani bao 1 - 0 katika
fainali iliyoonyeshwa moja
kwa moja (live) na televisheni
ya Azam.
Ilala ilifanikiwa kutwaa baada
ya kuichapa Kigoma mabao
3 -0 .

Bingwa amepata sh.
milioni tatu, makamu bingwa
sh. milioni mbili wakati
mshindi wa tatu ameondoka na
sh. milioni moja katika
michuano hiyo iliyodhaminiwa
na kampuni ya Proin .

MECHI ZA MWISHO FDL SASA
FEB 8 NA 10

Mechi za raundi mbili za
mwisho za Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) kwa makundi
yote mawili zimerudishwa
nyuma kutokana na maombi ya
klabu hizo kupungaza gharama
za kuendelea kuziweka
kambini timu zao .

Hivyo, Februari 8 mwaka huu
kundi A litacheza mechi zake
za raundi ya 21 wakati zile za
raundi 22 ambayo ndiyo ya
mwisho zitafanyika Februari 13
mwaka huu .

Mechi za Februari
8 ni KMC vs African Lyon ,
Kurugenzi vs African Sports,
Majimaji vs JKT Mlale,
Kimondo vs Friends Rangers,
Ashanti United vs Villa Squad,
Polisi Dar vs Lipuli.

Februari 13 mwaka huu ni
African Lyon vs Polisi Dar ,
Kurugenzi vs Lipuli, Kimondo
vs Majimaji, JKT Mlale vs
Ashanti United , Friends
Rangers vs African Sports, na
Villa Squad vs KMC .

Kwa upande wa kundi B
wataanza mechi za raundi 22
Februari 10 mwaka huu ili
kupisha mechi za viporo za
Polisi Mara zinazomalizika
Februari 5 mwaka huu .

Hivyo,
Februari 10 mwaka huu
itakuwa ni Burkina Faso vs JKT
Kanembwa , Mwadui vs Polisi
Tabora , Polisi Dodoma vs
Green Warriors, Rhino Rangers
vs JKT Oljoro, Panone vs Polisi
Mara , Geita Gold vs Toto
Africans

Raundi ya 22 itachezwa
Februari 15 mwaka huu kwa
mechi kati ya JKT Kanembwa
vs Green Warriors , Mwadui vs
Burkina Faso , Polisi Tabora vs
JKT Oljoro , Polisi Dodoma vs
Panone , Toto Africans vs Rhino
Rangers, na Geita Gold vs
Polisi Mara .

RAMBIRAMBI MSIBA WA
KATIBU IRFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania ( TFF) limepokea kwa
masikitiko taarifa ya msiba wa
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Iringa ( IRFA) , John Ambwene
Mwakalobo uliotokea jana
(Februari 1 mwaka huu )
mkoani Iringa baada ya
kuanguka akiwa nyumbani
kwake .

Msiba huo ni pigo kwa wadau
wa mpira wa mpira wa miguu
kwani wakati wa uhai wake ,
Mwakalobo alitoa mchango
mkubwa akiwa kiongozi .
Mwaka 2011 alichaguliwa
kuwa Makamu Mwenyekiti wa
IRFA , kabla ya 2012 kushinda
nafasi ya Katibu Msaidizi

Alizaliwa Februari 4 , 1954 na
kupata elimu ya sekondari
katika shule ya Azania, Dar es
Salaam na baadaye mafunzo ya
ualimu kwenye Chuo cha
Ualimu Mpwapwa mkoani
Dodoma. Alianzia kazi ya
ualimu Newala mkoani Mtwara
kabla ya kuhamia mkoani
Iringa mwaka 1981. Alistaafu
mwaka 2013 .

TFF inatoa salamu za
rambirambi kwa familia ya
marehemu , na Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa
Iringa ( IRFA) na kuwataka
kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu kwa
msiba huo .

Marehemu anatarajiwa
kuzikwa kesho ( Februari 3
mwaka huu ) kwao Kyela
mkoani Mbeya .
Ameacha mke,
watoto wanne na mjukuu
mmoja . Bwana alitoa, Bwana
ametwaa . Jina lake lihimidiwe .

 
FULU VIWANJA