Social Icons

Pages

Monday, 2 February 2015

FIFA YATAJA WAPINZANI WATATU WA BLATTER UCHAGUZI WA RAIS !

LEO FIFA imethibitisha kuwa
Rais wao Sepp Blatter
atagombea Urais kwa Kipindi
kingine cha Miaka Minne
akisimama pamoja na
Wagombea wengine Luis Figo,
ambae ni Fowadi wa zamani
wa Portugal, Michael van
Praag, Rais wa FA ya Holland,
na Mwana Mfalme wa Jordan ,
Ali Bin Al- Hussein.

Bodi ya Utawala ya FIFA
imetamka kuwa Wagombea
hao Wanne watapitia kwenye
tathmini ya Kimaadili kabla
hawajathibitishwa kama
Wagombea .

Mgombea mmoja, Jerome
Champagne, wa Ufaransa ,
alijitoa licha ya kutangaza
kugombea baada ya kushindwa
kupata Udhamini wa Vyama
Vitano vya Soka vya Nchi
Wanachama wa FIFA kama
taratibu za Uchaguzi
zinavyotaka .

Blatter , mwenye Miaka 78,
anawania Urais kwa Mara ya 5
tangu atwae wadhifa huo
Mwaka 1998 na anatarajiwa
kushinda tena kwenye
Uchaguzi utakaofanyika Mjini
Zurich , Uswisi Mei 29 Mwaka
huu .

Licha ya kupingwa na kupigwa
madongo na Nchi za Ulaya,
hasa baada ya England
kubwagwa katika azma yake
ya kuwa Mwenyeji wa Fainali
za Kombe la Dunia za Mwaka
2018 na 2022 ambazo
wamepewa Russia na Qatar ,
Blatter anatarajiwa
kuchaguliwa tena kuwa Rais
wa FIFA.

Blatter anategemewa kuzoa
Kura toka Asia , Afrika na
Marekani ya Kusini ambao
ndiko waliko Wanachama
wengi wa FIFA ukilinganisha na
53 wa Ulaya kati ya
Wanachama 209 Duniani.

 
FULU VIWANJA