Social Icons

Pages

Monday, 2 February 2015

GERVINHO WAIPELEKA IVORY COAST NUSU FAINALI, KUCHEZA NA CONGO DR!

JANA huko Nuevo Estadio de
Malabo , Mjini Malabo Nchini
Equatorial, Mchezaji mpya wa
Manchester City, Wilfried Bony ,
na yule wa zamani wa Arsenal,
Gervinho , ambae sasa yupo AS
Roma walipachika Mabao
yaliyoipeleka Nchi yao Ivory
Coast Nusu Fainali ya AFCON
2015 , Kombe la Mataifa ya
Afrika, walipoitwanga Algeria
Bao 3 - 1.

Bony alifunga Bao la kwanza
Dakika ya 26 kwa Kichwa
alipounganisha Krosi ya Max
Gradel lakini Hilal Soudani
akaisawazishia Algeria Dakika
ya 51 na ndipo Bony akafunga
tena kwa Kichwa Bao la Pili
alipounganisha Frikiki ya Yaya
Toure katika Dakika ya 69.

Bao la 3 lilifungwa na Gervinho
katika Dakika ya 90

Kwenye Nusu Fainali,
Jumatano ni Congo DR v Ivory
Coast na Alhamisi ni Equatorial
Guinea v Ghana .

 
FULU VIWANJA