Kocha wa Real
Madrid, Carlo
Ancelotti sasa
atakuwa na amani
moyoni kwa kuwa
beki wake, Pepe
amerejea.
Kwa mujibu wa
kitengo cha afya cha
Real Madrid, Pepe
sasa yuko poa na
anaweza kucheza
mechi zinazofuata.
Pepe ambaye kuumia
kwake kulifanya safu
ya ulinzi ya Real
Madrid iyumbe
kinoma, sasa
amerejea.
Amekuwa akiaminika
kama kiongozi wa
safu ya ulinzi ya
Madrid akisaidiana
na Sergio Ramos.
Jumatano, Madrid
itakuwa na kazi
ngumu ya kuivaa
Schalke 04 ya
Ujerumani na
watakuwa na nguvu
zaidi kutokana na
kurejea kwa beki
huyo kisiki.