Timu ya Taifa ya
Tanzania ya Mpira wa
Miguu wa Ufukweni
(Beach Soccer) jana
imeibuka na ushindi
wa mabao 5- 3
ugenini dhidi wa
wenyeji timu ya Taifa
ya Kenya kwenye
mchezo uliofanyika
kwenye Uwanja wa
fukwe za Hotel ya Big
Tree Pirates jijini
Mombasa.
Katika mchezo huo
mabao ya Tanzania
yalifungwa na Ali
Rabbi mabao manne
na Mwalimu Akida
bao moja .
Kipindi cha kwanza
kilimazika kwa
Tanzania kupata
mabao 2 Kenya 1,
kipindi cha pili
kilimalizika Tanzania
4 Kenya 3 na kipindi
cha tatu na cha
mwishokwa mchezo
kimalizika kwa
Tanzania kupata
mabao 5 Kenya 3.
Mechi ya marudiano
inatarajiwa kuchezwa
jumamosi wiki hii
Februari 21, 2015
jijini Dar es salaam,
na endapo timu ya
Taifa ya Tanzania
itafanikiwa kuwatoa
Kenya, itacheza na
timu ya Taifa ya Misri
katika hatua
inayofuata.
Mchezo wa kwanza
utafanyika kati ya
tarehe 7,8 Machi
2015 jiji Dar es
salaam na marudiano
yatafanyika nchini
Misri kati ya tarehe
13,14 Machi 2015.
Timu inarejea leo
jijini Dar es salaam
majira ya saa 11 jioni
ikitokea jijini
Mombasa nchini
Kenya.