Social Icons

Pages

Saturday, 31 January 2015

TAIFA CUP WANAWAKE- FAINALI: PWANI v TEMEKE, AZAM COMPLEX , KIINGILIO BURE, WAZIRI MUKANGARA MGENI RASMI!

Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk
Fenella Mukangara atakuwa
mgeni rasmi kwenye fainali ya
michuano ya Kombe la Taifa
Wanawake kati ya Pwani na
Temeke itakayochezwa Uwanja
wa Azam Complex uliopo
Chamazi jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo itakayoanza saa
10. 15 jioni itachezeshwa na
mwamuzi wa FIFA , Jonesia
Rukyaa , na itaonyeshwa moja
kwa moja na televisheni ya
Azam. Waamuzi wasaidizi ni
Hellen Mduma , Agnes
Alphonce , na Mwanahamisi
Matiku wakati Kamishna ni
Ingridy Kimario.

Timu za Ilala na Kigoma
zitacheza mechi ya utangulizi
kutafuta mshindi wa tatu
kuanzia saa 8 .00 mchana.
Bingwa wa michuano hiyo
inayodhaminiwa na kampuni ya
Proin na kufanyika kwa mara
ya kwanza nchini atapata
kombe na sh. milioni tatu.

Makamu bingwa atapata sh .
milioni mbili wakati mshindi
wa tatu atapata sh. milioni
moja .

Kiingilio kwenye mechi hizo ni
bure.

 
FULU VIWANJA