Social Icons

Pages

Saturday, 31 January 2015

TETESI BARANI ULAYA

Hizi ndizo habari za uhamisho wa
wachezaji ambazo zimezungumziwa
sana siku ya Ijumaa
YAYA TOURE

Kocha wa Inter Milan Roberto
Mancini amesema anatamani
kumsajili kiungo wa Manchester City
Yaya Toure mwenye miaka 31 baada
ya kuonekana hakuna mwelekea
kuhusu mkataba mpya.
(Sky Sports)
PABLO ALCACER:

Mshambuliaji wa Valencia Pablo
Alcacer mwenye miaka 21 amesema
ndoto yake ilikua kusaini mkataba
mpya wa Valencia ambao ameusaini
licha ya kutakiwa na Liverpool.
(Talksport)
KEVIN MIRALAS

Matumaini ya Tottenham Hottspurs
kumsajili winga wa Everton Kevin
Mirallas, 27 kabla ya kufungwa
dirisha la usajili yanazidi
kuongezeka na katika dili hilo
atahusishwa pia Aaron Lenon
ambaye ataenda Everton.
(Daily Mirror)
JUAN COADRADO

Dili la Chelsea kumsaini winga wa
Fiorentina Juan Cuadrado, 26,
linafikia katika hatua nzuri na
atatangazwa rasmi muda wowote
kama mchezaji wa Chelsea ambapo
pia itamhusisha Andre Schurrle, 24,
kwenda  Wolfsburg akitokea Chelsea
(Daily Mail)
ENNER VALENCIA:

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
pia anataka kupeleka paundi milioni
21 kumsajili mshambuliaji wa West
Ham Enner Valencia mwenye miaka
25.
(Sun )
SAMI KHEDIRA:

Klabu ya Trabzonspor imepewa
nafasi kubwa kumsajili kiungo wa
Real Madrid Sami Khedira mwenye
miaka 27 ambaye pia anawaniwa na
klabu nyingi za ligi kuu ya England.
.(Daily Star)
YOUNES KABOUL:

Tottenham hotspurs wako tayari
kumtoa nahodha wake  Younes
Kaboul, 29, ambaye pia hucheza
kama Beki wa kati ili kumpata
mshambuliaji kinda wa Stuttgart
Timo Werner mwenye miaka 18.
(Daily Mirror)
ANDERSON:

Mazungumzo yanaendelea kati ya
Manchester United na Internacional
ya Brazil ili kusajiliwa kwa kiungo
Anderson, 26, ambaye maisha yake
katika klabu ya Manchester United
hayaeleweki.
(Daily Telegraph)
DIEGO FORLAN

West Brom wamepewa nafasi ya
kumsajili mshambuliaji wa zamani
wa Manchester United  Diego Forlan,
35, kwa mkopo toka klabu ya Japan
Cerezo Osaka.
(Express,Star, Wolverhampton)

 
FULU VIWANJA