Social Icons

Pages

Tuesday, 20 January 2015

SENAGAL WAIBAMIZA GHANA

Senegal yaichapa Ghana
Mshambuliaji wa Senegal Moussa
Sow alifunga bao la mda wa lala
salama na kuisaidia Senegal kupata
ushindi dhidi ya Black stars ya
Ghana.

Mchezaji huyo aliyeingia dakika za
mwisho za mechi hiyo alifunga bao
lake kunako dakika ya 90 na kuipatia
timu yake alama zote tatu.
Mchezaji wa Ghana Andrew Ayew
alifunga mkwaju wa Penalti baada ya
kiungo wa kati wa Everton Christian
Atsu kuangushwa katika eneo la
hatari.

Lakini Senegal ilijitahidi na kupiga
chuma cha goli la Ghana kupitia
mchezaji Kara Mbodj,kabla ya
mshambuliaji wa Stoke Mame Biram
Diouf kufunga bao la kusawazisha
huku Mousa Sow akifunga bao la
Ushindi.

 
FULU VIWANJA