Social Icons

Pages

Wednesday, 21 January 2015

ARSENAL YAKUTANA NA ZAIDI YA MAKAMPUNI 20 NCHINI



Kama maofisa biashara wa Klabu ya Arsenal wakifikia makubaliano mazuri na zaidi ya makampuni 20 ya hapa nchini, basi timu shiriki za Ligi Kuu Bara, zikiwemo Simba na Yanga zitafaidika kwa udhamini kutoka kwao.

hayo yamesemwa na moja ya maofisa ,Willey amesema wamepanga kukutana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya soka katika kuhakikisha wanapiga hatua.

Aliongeza kuwa ni ngumu moja kwa moja kukubali kuzisaidia klabu za ligi kuu kutokana na bodi maalum Arsenal inayohusiana na maendeleo, hivyo hadi watakapokaa pamoja kujadiliana ndiyo watatoa maamuzi.

“Tupo hapa nchini kwa ajili ya kutengeneza masuala ya kibiashara kati yetu Arsenal na makampuni ya hapa nchini, tulishaanza nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Nigeria, Kenya, Misri, Afrika Kusini na nyingine nyingi ambazo tunauza vifaa mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi zetu kwa njia ya mtandao (online).


“Katika kujenga uhusiano huo, tupo tayari kuzisaidia klabu za hapa nchini zinazoshiriki ligi kuu, lakini hadi kutakapokuwepo makubaliano mazuri kati yetu na kampuni 20, tulizopanga kufanya nazo biashara, tupo kwenye hatua nzuri za kukamilisha mpango,” alisema Willey.
 
FULU VIWANJA