Social Icons

Pages

Monday, 19 January 2015

ANDY MURRAY AMEANZA KWA USHINDI HUKO MELBOURNE

Mcheza tenesi Andy Murray ameanza
michuano ya wazi ya Melbourne,kwa
ushindi baada ya kumchapa Yuki
Bhambri.

Murray ameanza kwa ushindi huo
kwa kushinda seti 6-3 6-4 7-6 (7-3)
katika mchezo uliotumia saa na
dakika kumi na mbili katika uwanja
wa Margaret Court.

Murray mwenye miaka 27, alianza
kwa kupoteza seti ya kwanza kwa
kuchapwa 4-1 kabla ya kurudi na
kufanikiwa kuibuka mshindi.
"Nafikiri ni mwanzo mzuri, mpinzani
wangu alicheza vizuri na
kushambulia vizur katika mchezo
wote.

Yuki Bhambri ameweza kutoa
upinzani wa kutosha kwa Murray japo
kuwa yuko chini sana katika viwango
vya tenesi akishika nafasi ya 317
katika ubora wa dunia .

Murray atakabiliana na Marinko
Matosevic wa Australia katika
mchezo unaofuata siku ya Jumatano.

Huku nyota mwingine wa tenesi
Rafael Nadal nae akimshinda Mikhail
Youzhny,
Nadal ameshinda kwa 6-3 6-2 6-2
katika mchezo wake wa kwanza toka
alipokosa michezo ya Wimbledon
kutokana na kuwa majeruhi.

Kwa upande wa wanawake Ana
Ivanovic alishangazwa na Lucie
Hradecka Jamuhuri ya Czech.kwa
kukubali kuchapwa 1-6 6-3 6-2 .

 
FULU VIWANJA