Social Icons

Pages

Saturday, 24 January 2015

RONALDO APEWA NYEJUNDU,BENZEMA NA BALE WAENDELEA KUIPAISHA MADRID :LA LIGA

Real Madrid Leo wamepata
ushindi wa jasho wa Bao 2- 1
walipocheza Ugenini huko
Estadio Nuevo Arcángel Mjini
Córdoba kwa kuichapa Cordoba
huku Bao la ushindi likifungwa
Dakika ya 89 kwa Penati ya
Gareth Bale.

Real walicheza Mtu 10 kuanzia
Dakika ya 82 kufuatia Kadi
Nyekundu kwa Mchezaji Bora
Duniani, Cristiano Ronaldo,
kwa kuinua mkono wake na
kudaiwa kumpiga usoni
Edimar .

Cordoba ndio waliotangulia
kupata Bao katika Dakika ya
Pili tu kwa Penati ya Ghilas
baada ya Sergio Ramos
kuunawa Mpira lakini Karim
Benzema akaisawazishia Real
katika Dakika ya 27 .

Ushindi huu umewapaza Reak
kuwa Pointi 4 mbele ya Timu
ya Pili Barcelona huku wote
wakiwa wamecheza Mechi
sawa ingawa Barca baadae
Leo watacheza Mechi yao ya
La Liga Ugenini na Elche .

 
FULU VIWANJA