Kilabu ya Uhispania Villareal
imethibtisha makubaliano na Arsenal
kuhusu uhamisho wa beki Gabriel
Paulista katika uwanja wa Emirates.
Katika makubaliano hayo Arsenal
kwa upande wake itamtoa kwa mkopo
mshambuliaji wake Joel Campbell
kwa Villareal.
Bado kuna maelezo machache katika
makubaliano hayo ili yaweze
kuafikiwa rasmi na yanatarajiwa
kutiwa sahihi siku ya
jumatatu ,ambapo beki huyo wa
Brazil atafanyiwa ukaguzi wa
matibabu kabla ya kuweka sahihi
yake na kilabu ya Arsenal.
Mlinzi huyo wa miaka 24 ambaye
alijiunga na kilabu hiyo ya La liga
mwaka 2013 amekuwa kiungo
muhimu wa manuwari hiyo ya
manjano na ameweza kuiwakilisha
kilabu hiyo mara 50.