Maajabu ya kombe la FA pale
England yameendelea kuonekana
baada ya jana Manchester United
United kutoka sare ya bila kufungana
na timu ya daraja la pili ya
Cambridge United leo michezo
kadhaa imepigwa na kushuhudiwa
vigogo wa ligi ya England wakitupwa
nje.
Mechi hizo za Raundi ya nne
zimemalizika muda mfupi uliopita na
kushuhudiwa Vinara wa Ligi Kuu
England Chelsea wakitupwa nje kwa
kufungwa bao 4-2 nyumbani kwao
Stamford Bridge na klabu ya daraja
la Championship Bradford City.
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu
Nchini England Manchester City wao
walikubali kichapo cha bao 2-0
nyumbani Etihadi toka kwa
Middlesbrough timu nyingine
inayoshiriki Championship.
Southampton ambao msimu huu
wameonekana wako vizuri na
kushika nafasi ya tatu katika
msimamo wa Ligi walikubali kichapo
cha bao 3-2 toka kwa Crystal Palace
ambayo imeongezwa nguvu kufatia
kumpata kocha mpya Allan Pardew
pambano hilo lilipigwa nyumbani
kwa Southamptob St. Marys
stadium.
Klabu zingine za Ligi kuu ambavyo
vimepata vichapo leo ni pamoja na
Swansea City waliokubali kichapo
cha bao 3-1 toka kwa Blackburn
Rovers ambayo nayo inashiriki Ligi
ya Championship.
Blackburn Rovers
3-1 Swansea
Birmigham City 1-2
West Brom
Cardiff City 1-2
Reading
Chelsea 2-4
Bradford City
Derby County 2-0
Chesterfield
Manchester City 0-2
Middlesbrough
Preston 1-1
Sheffield United
Southampton 2-3
Crystal Palace
Sunderland 0-0
Fulham
Tottenham Hotspurs
1-2 Leicester City
Patrick Blo