Mark Clattenburg ndie
ameteuliwa kuchezesha ule
mtanange wa Jumamosi
Uwanjani Stamford Bridge kati
ya Vinara wa Ligi Kuu England
Chelsea na Mabingwa Watetezi
wa Ligi hiyo Manchester City .
Chelsea wanaongoza Ligi
wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu
ya Pili Man City .
Refa Clattenburg ni mmoja wa
Marefa Wawili wa England
ambao wapo kwenye kiwango
cha juu kabisa cha Urefa cha
UEFA na mwingine ni Martin
Atkinson .
Lakini Refa huyo ameshawahi
kulalamikiwa na Klabu zote
hizo mbili huko nyuma.
Bosi wa Man City, Manuel
Pellegrini anaetokea Nchini
Chile , ameshawahi kudai
Clattenburg aliwakosesha
ushindi walipotoka Sare 2 - 2 na
Arsenal Mwezi Septemba huko
Emirates na Msimu uliopita
Pellegrini pia alimwandama
Refa huyo wakati walipofungwa
3 -2 na Liverpool.
Chelsea pia wana historia ya
uhasama na Clattenburg ambae
waliwahi kumsakama na
kumshitaki kwa kumkashifu
Kibaguzi Kiungo wao John Obi
Mikel wakati wa Mechi ya Ligi
dhidi ya Manchester United
Mwezi Oktoba Mwaka 2012 .
Hata hivyo , baadae , FA, Chama
cha Soka England , kilimsafisha
Refa huyo kuhusu tuhuma hizo.
LIGI KUU ENGLAND