Social Icons

Pages

Tuesday, 27 January 2015

AFCON 2015: KUNDI D BALAA, MAOMBI YA CITY YAYA TOURE AIWAHI CHELSEA JUMAMOSI KUAMULIWA KWA KURUSHWA SHILINGI?

MATUMAINI ya Manchester
City kumpata Mchezaji wao
Yaya Toure kucheza Mechi yao
ya Jumamosi dhidi ya Chelsea
huenda yakaamuliwa kwa
kurushwa Sarafu kwa vile Nchi
ya Toure, Ivory Coast,
imefungana kila kitu na Timu
nyingine zote kwenye Kundi D
la Mashindano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika, AFCON 2015.

Mechi zote za Kundi D huko
Nchini Equatorial Guinea
zilimalizika kwa Sare ya 1- 1
hivyo kila Nchi, Ivory Coast,
Cameroun, Guinea na Mali zina
Pointi 2 kila mmoja na kila
mmoja amefunga Bao 2 na
kufungwa 2 .

 
FULU VIWANJA