Mshambuliaji wa Everton Samuel
Eto'o amejiunga rasmi na klabu ya
Sampdoria ya Italia na kusa mkataba
wa miaka mitatu na nusu
utakaomweka klabuni hapo mpaka
mwaka 2018.
Samuel Eto'o mwenyewe ameweka
picha katika aksunti yake ya Twitter
ikiwa na maneno
"Vipimo vya afya
vimekamilika na sasa niko tayari
kwa changamoto mpya"
Nahodha huyo wa zamani wa
Cameruni mwenye miaka 33
alijiunga na Everton kiwa mchezaji
huru mwaka jana mwezi Agosti na
kufunga magoli manne katika mechi
20 alizoichezea Everton katika
mashindano yote.
Katika taarifa ya kocha wa Everton
Roberto Martinez alimshukuru Eto'o
kwa mchango wake alioutoa katika
klabu hiyo hasa akiwa mhamasishaji
mkubwa kwa vijana katika mechi za
Ulaya na kumtakia mafanikio mema
aendako.
Hii ni mara ya pili Eto'o anaenda
Italia baada ya kujiunga na Inter
Milan mwaka 2009 ambapo alifunga
magoli 25katika miaka miwili
aliyocheza Inter Milan.
msimu uliopita Eto's aliichezea
Chelsea na katika mkataba wake wa
mwaka mmoja ambapo alifunga
magoli 12 katikamechi 35.