Social Icons

Pages

Monday, 19 January 2015

MANUEL PELLEGRIN AMESEMA LAZIMA TUIFUNGE CHELSEA.

Manuel Pellegrini amekiri kuwa
kama Manchester City wanataka
kuteteta ubingwa wa ligi kuu England,
EPL, lazima waifunge Chelsea.
Pellegrini amesema hayo kufuatia
kuambulia kipigo cha mabao 2-0 dhidi
ya Arsenal katika mechi ya ligi kuu
iliyopigwa jana uwanja wa Etihad.

City walifungwa na Santi Cazorla kwa
mkwaju wa penalti katika dakika ya
24, na baadaye mshambuliaji aliye
kwenye ubora Olvier Giroud aliandika
bao la pili kwa njia ya kichwa dakika
ya 67.

Kipigo hicho kimewafanya Man City
wawe pointi tano nyuma ya Chelsea
ambao waliifunga Swansea mabao 5-0
jumamosi iliyopita.

Man City watasafiri januari 31 mwaka
huu kwenda Stamford Bridge ambapo
watachuana na wenyeji Chelsea.

“Lazima tupunguze pengo mpaka
kufikia mbili. Natumaini tutarudi
katika kiwango chetu cha kawaida.

” Mchezo wa Chelsea utakuwa
mgumu sana. Tutajitahidi kushinda
mechi hiyo kupunguza pengo la
pointi”.

 
FULU VIWANJA