JANA
Usiku huko Nuevo Estadio de Malabo, Mjini Malabo katika Mechi ya pili
ya Kundi D la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, Mali na
Cameroun zilitoka Sare ya Bao 1-1.Ambroise Oyongo aliokoa kipigo Cameroun baada ya kusawazisha katika Dakika ya 84 kufuatia Bao la Dakika ya 70 la Mali lilifungwa na Sambou Yatabare
Mapema Jana kwenye Uwanja huo huo, Ivory Coast na Guinae zilitoka Sare 1-1 katika Mechi ya kwanza ya Kundi D.