Social Icons

Pages

Sunday, 25 January 2015

IVORY COAST WAPATA USHINDI DAKIKA ZA JIONI..

Mchezaji Max Gradel wa Ivory Coast
alifunga bao la dakika za mwisho la
kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya
Mali na hivyobasi kuimarisha
matumaini yao ya kufuzu katika robo
fainali ya michuano ya mataifa ya
Afrika.

Mali ilikuwa kifua mbele huku ikiwa
na ishara zote za kuibuka mshindi
baada ya Bakary Sako kufunga bao
zuri kunako dakika ya saba ya kipindi
cha kwanza.

Lakini Gradel alisawazisha katika
dakika ya 86 ndani ya eneo la hatari.

Awali Ivory Coast ilinyimwa penalti
ya wazi baada ya Wilfried Bonny
kuchezewa visivyo na Molla Wague
huku Kolo Toure pia akikosa bao la
wazi.

 
FULU VIWANJA