Mchezaji bora wa soka duniani
Cristiano Ronaldo alikataa kusajiliwa
na kilabu ya Arsenal kwa kuwa bei ya
kuujenga uwanja wa Emirates wakati
huo uliiwacha kilabu hiyo bila senti.
Mchezaji huyo wa Real Madrid
aligunduliwa na The Gunners lakini
Manchester United ikamsajili mwaka
2003.
Wakala wa Ronaldo Jorge Mendes
amesema kuwa gharama ya uwanja
wa Emirates uliondoa fursa ya
Arsenal kumsajili mchezaji huyo.
Katika kitabu chake kipya Mendes
anasema kuwa kuna wakati ambapo
alidhani Ronaldo atajiunga na
Arsenal .
''David Dein ni mtu mzuri sana lakini
kutokana na kujengwa kwa uwanja
wa Emirate ,kilabu hiyo haikuwa na
fedha na haikuwezekana kumsajili
Ronaldo'',alisema Mendes..