LIGI KUU VODACOM imendelea
Leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar
es Salaam kwa Mechi pekee
ambayo Simba ilichapwa 2- 1
Mbeya City lakini stori kubwa
ni Simba kukosa Penati Dakika
ya mwisho ambayo ingewapa
Sare .
Simba walitangulia kufunga
Bao katika Dakika za Majeruhi
za Kipindi cha Kwanza kwa
Frikiki ya Ibrahim Hajib na
Mbeya City kusawazisha
Dakika ya 77 Mfungaji akiwa
Hamad Kibopile .
Mbeya walipata Bao lao la
ushindi Dakika za Majeruhi
kwa Penati iliyofungwa na
Yusuf Abdallah kufuatia Kipa
Peter Manyika kumchezea Rafu
Raphael Daudi.
Mara tu baada ya Bao hilo
Simba walipata nafasi ya
kutoka Sare baada ya Refa
Abadallah Kambua kutoa Penati
kwa Rafu aliyochezewa Jonas
Mkude lakini Nassor Masoud
‘Chollo ’ alifumua Shuti
lililopiga Posti na kuleta
kizaazaa kwa Mashabiki wa
Simba.
Matokeo haya yameiacha
Simba ikiwa Nafasi ya 11 , 4 tu
toka mkiani na Mbeya City
kukwea hadi Nafasi ya 7
Mechi zinazofuata za VPL
zitachezwa Jumamosi na
Jumapili .