Basi la Timu ya Taifa ya Tanzania limekombolewa na TFF
SHIRIKISHO la Soka Tanzania
(TFF), limefanikiwa kulikomboa basi la timu ya soka la wanaume ya
Tanzania, ‘Taifa Stars,’ huku likikiri kupata usumbufu mkubwa wa deni
la kurithi la shilingi mil. 140 lililosababisha kukamatwa kwa chombo
hicho ghali
Basi kubwa la Taifa Stars aina ya
Yutong lililotolewa na wadhamini wa Taifa Stars, Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager,
lilikamatwa katikati ya mwaka jana kwa agizo la Mahakama, ambapo TFF
ilitanguliza sh. Mil 70.
Akizungumza na mwandishi wetu
jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine, amesema
harakati mbalimbali za ndani na nje ya Mahakama, zimefanikisha
kukombolewa kwa basi hilo na sasa liko mikononi mwao tayari.
“Hili ni suala la kisera na
lilipaswa kuzungumzwa na Rais wa TFF, lakini kifupi ni kwamba tumemaliza
kulipa deni husika ambalo TFF yetu ilirithi kutoka kwa TFF iliyopita,
hivyo tumelikomboa rasmi basi hilo na liko mikononi mwetu,” Amesema
Mwesigwa.
Mwesigwa amesema kuwa, kimsingi
deni hilo liliwapa wakati mgumu na hawakuwa na njia ya kutolilipa baada
ya kulirithi na kwamba liliwaumbua vya kutosha, ingawa wanashukuru kwa
jitihada zao za kulikomboa kuzaa matunda.
Source: hivisasa.co.tz