Beki wa Celtic, Virgil van Dijk (katikati) amefungua milango ya kwenda EPL
DILI
la Arsenal kumnunua Virgil van Dijk linaweza kukamilika kufuatia beki
huyo wa Celtic kuonesha nia ya kuzungumza na klabu za ligi kuu England,
EPL kama zitatoa ofa mwezi huu.
Celtic
wanasisitiza kuwa hawataki kumuachia beki huyo labda kama kutakuwa na
dau kubwa, lakini Van Dijk ametaja umri wake kuwa sababu kubwa ya
kuhitaji kuondoka.

“Kwasasa nimeanza kuwaza kuhusu hilo (maisha ya baadaye),” Van Dijk aliwaambia De Telegraaf.
“Nina umri
wa miaka 23 sasa na nimecheza Willem II, FC Groningen na Celtic na sasa
nahusishwa na klabu kama Arsenal. Sio jambo kubwa?
“Kuna
klabu nyingi zinavutiwa na mimi, lakini Celtic wanaweka ngumu wakitaka
ada kubwa ya usajili. Klabu ipo sawa: hawataki kuniachia majira ya
baridi kwasababu tunacheza makombe manne.
