Timu ya taifa ya Australia imeshinda
bao 2-0 wakiifunga United Arab
Emirates (Umoja wa Falme za
Kiarabu) na kutinga katika fainali ya
kombe la mataifa ya Asia kwa mara
ya pili mfululizo.
Katika mchezo huo uliopigwa katika
dimba la Newcastle lililojaa maji
kutokana na mvua inayoendelea
kunyesha Nchini Australia wenyeji
Australia ambao ni waandaaji wa
michuano hiyo mwaka huu walipata
mabao yao mawili katika dakika 14
tu tangu mchezo ulipoanza mabao
ambayo yalidumu mpaka mwisho wa
mchezo.
Australia ilipoteza katika fainali ya
michuano hiyo miaka minne iliyopita
wakifungwa na Japan watatakiwa
kukomaa na kubakiza kombe mwaka
huu watakapoikabili Korea Kusini
Katika Fainali ya mwaka Huu
itakayopigwa katika jiji la Sydney
Jumamosi hii.
Australia ilipata magoli yake kupitia
kwa Trent Sainsbury dakika ya 3
badae Jason Davidson akiongeza la
pili dakika ya 11 ikiwaacha UAE
wakipoteza nafasi ya kufika fainali
baada ya kufika Nusu fainali kwa
mara ya kwanza tangu mwaka 1996.
Korea Kusini imeingia katika fainali
katika mechi ya awali walipoifunga
Iraq bao 2-0 katika mechi ya awali
siku ya jana.