MABINGWA wa Spain Atletico
Madrid Jana Usiku walitupwa
nje ya Copa del Rey baada ya
kuchapwa Bao 3 -2 na
Barcelona katika Mechi ya
Marudiano iliyochezwa Vicente
Calderon huku Bao zote
zikifungwa kabla ya Haftaimu
na Atletico kumaliza Mechi
wakiwa Mtu 9.
Katika Mechi ya Kwanza
iliyochezwa Nou Camp Wiki
iliyopita, Barcelona waliibuka
washindi kwa Bao 1 -0 kwa Bao
la Dakika ya 85 la Staa wao
Lionel Messi ambalo alilifunga
baada ya Penati yake
kuokolewa na Kipa na Mpira
kumrudia tena na kuukwamisha
wavuni na hivyo Barcelona
kusonga Nusu Fainali kwa
Jumla ya Mabao 4 -2 na
watakutana na Mshindi kati
Getafe na Villareal ambao
katika Mechi yao ya kwanza,
Villareal alishinda Bao 1- 0 .
Kwenye Mechi ya Jana,
Fernando Torres aliipa Atletico
Bao la kuongoza na Neymar
kusawazisha.
Kisha Penati ya Raul Garcia
ikawapa Atletico Bao la Pili
lakini Beki wao Miranda
akajifunga mwenyewe na
Neymar akaipa Barca Bao la 3
na la ushindi .
Balaa kwa Atletico lilikuja pale
Gabi alipopewa Kadi Nyekundu
wakati wa Haftaimu Wachezaji
wakielekea Vyumba vya
Kubadili Jezi na Mario Suarez
kufuatia mwishoni.