Social Icons

Pages

Monday, 12 January 2015

ARSENAL WAANZA MAKEKE YA USAJILI KWA KUTAZAMIA HUKO UJERUMANI

Klabu ya arsenal tayari imeanza
mazungumzo rasmi ya kumuwania
Kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay
Gundogan huku kiasi ya Pauni 16M
zikitajwa kuhitajika katika usajili
huo.
Arsenal wamekuwa na tatizo la kiungo
mkabaji kwa muda sasa tangu
kuondoka kwa Alex Song aliyetimkia
Barcelona na nafasi hiyo kucheza na
Aaron Ramsey, Mikel Arteta na
Methew Flamin huku wote
wakionekana kupwaya.
Pamoja na kufanya mazungumzo ya
kumnasa kiungo huyo, Gunners
wametajwa pia na magazeti ya leo
barani Ulaya kumuhitaji mshambuliaji
wa klabu ya PSG, Ednison Cavani
ambaye anaonekana kuto ridhika na
namna mambo yanavyoendelea kwa
mabingwa hao wa Ufaransa.
Kumpata Cavani kutaongeza nguvu
kwenye safu ya ushambuliaji ya
Arsenal inayoongozwa na Alexies
Sanchez ambaye amefunga magoli 10
ya ligi kuu mpaka sasa.
Kwa upande mwingine, Arsenal
wanaonekana kumuwinda kipa wa
Chelsea Peter Cech na kula dalili za
kumpata baada ya msimu huu
kumalizika.

 
FULU VIWANJA